Pular para o conteúdo
Publicidade

A fé vem pelo ouvir

Por Bíblia Online

A fé vem pelo ouvir, e o ouvir pela Palavra de Cristo. Quando a Palavra é proclamada, a fé nasce nos corações. Ouvir a Deus é o primeiro passo para crer e seguir.

A fé vem pelo ouvir

A fé vem pelo ouvir, e o ouvir pela Palavra de Cristo. Quem ouve a Palavra crê e obtém a salvação eterna.

Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. Kwa maana, "Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa."

Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, "Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!"

Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, "Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?" Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia?

Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho Mtakatifu mliyeahidiwa, yeye ambaye ni amana yetu akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake.

"Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.

Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai.

Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. Imeandikwa katika Manabii, Wote watafundishwa na Mungu.Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu. Hakuna mtu yeyote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba. Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele.

Ouvir e obedecer

Felizes os que ouvem a Palavra de Deus e a praticam. Quem tem ouvidos ouça o que o Espírito diz.

Yesu akajibu, "Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii."

Mwenye masikio ya kusikia, na asikie."

Akawaambia, "Enendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema:

" Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

na pia mtatazama lakini hamtaona.

Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

hawasikii kwa masikio yao,

na wamefumba macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

na kugeuka nami nikawaponya.

Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia.

Vitu Vitiavyo Unajisi

Yesu akaita ule umati wa watu, akawaambia, "Sikilizeni na mwelewe:

Tegeni sikio mje kwangu,

nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi.

Nitafanya agano la milele nanyi,

pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.

Akasema, "Nenda ukawaambie watu hawa:

" Mtaendelea daima kusikiliza,

lakini kamwe hamtaelewa;

mtaendelea daima kutazama,

lakini kamwe hamtatambua.

Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu,

fanya masikio yao yasisikie,

na upofushe macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

nao wakageuka, nikawaponywa."

Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.

Seja o primeiro