Pular para o conteúdo
Publicidade

A última palavra vem do Senhor

Por Bíblia Online

A última palavra pertence ao Senhor. Os planos do homem estão sujeitos à soberania de Deus. Ele rege toda a história e nenhum de seus propósitos pode ser frustrado.

Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,

bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe;

hata waovu kwa siku ya maangamizi.

Mungu si mtu, hata aseme uongo,

wala yeye si mwanadamu, hata ajute.

Je, anasema, kisha asitende?

Je, anaahidi, asitimize?

Bwana akamjibu Mose, "Je, mkono wa Bwana ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la."

ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu:

Halitanirudia tupu,

bali litatimiliza lile nililokusudia

na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.

"Mimi ndimi Bwana, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza?

"Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

Bwana hufanya lolote apendalo,

mbinguni na duniani,

katika bahari na vilindi vyake vyote.

Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.

Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Hili jambo linakuja! Hakika litatokea, asema Bwana Mwenyezi. Hii ndiyo siku ile niliyosema habari zake.

Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. Badala yake, inawapasa kusema, "Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile."

Seja o primeiro