Pular para o conteúdo
Publicidade

A última palavra vem do Senhor

Por Bíblia Online

A última palavra pertence ao Senhor. Os planos do homem estão sujeitos à soberania de Deus. Ele rege toda a história e nenhum de seus propósitos pode ser frustrado.

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;

Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake;

Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.

Mungu si mtu, aseme uongo;

Wala si mwanadamu, ajute;

Iwapo amesema, hatalitenda?

Iwapo amenena, hatalitimiza?

BWANA akamwambia Musa, Je! Mkono wa BWANA umepungua urefu wake? Sasa utaona kama neno langu litatimizwa kwako, au la.

ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?

Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote,

Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.

BWANA amefanya kila lililompendeza,

Katika mbingu na katika nchi,

Katika bahari na katika vilindi vyote.

Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU; hii ndiyo siku ile niliyoinena.

lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.

Seja o primeiro