Publicidade

O adultério

Por Bíblia Online

O adultério é pecado grave que destrói alianças, famílias e vidas. A Bíblia condena firmemente a infidelidade conjugal e chama à pureza, fidelidade e santidade no casamento.

A lei de Deus

Não adulterarás. Quem comete adultério destrói a própria alma. A Palavra de Deus é clara e direta sobre este pecado.

Usizini.

" Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe.

" Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.

Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;

yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.

Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;

yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.

Mapigo na aibu ni fungu lake

na aibu yake haitafutika kamwe;

kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,

naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.

Hatakubali fidia yoyote;

atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.

Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake

bila nguo zake kuungua?

Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka

bila miguu yake kuungua?

Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;

hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.

Jesus ensina

Quem olhar para uma mulher com intenção impura já adulterou no coração. Jesus elevou o padrão da pureza.

Kuhusu Uzinzi

"Mmesikia kwamba ilinenwa, Usizini. Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.

Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.

Akawajibu, "Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini."

"Mtu yeyote amwachaye mkewe na kumwoa mwanamke mwingine anazini, naye mwanaume amwoaye mwanamke aliyetalikiwa anazini.

Wakamwambia Yesu, "Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?" Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki.

Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, "Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe." Akainama tena na kuandika ardhini.

Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. Yesu akainuka na kumwambia, "Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?"

Yule mwanamke akajibu, "Hakuna hata mmoja Bwana."

Yesu akamwambia, "Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena."]

Armadilhas e consequências

Os lábios da mulher estranha destilam mel, mas o seu fim é amargo. Fuja da imoralidade — o adultério escraviza.

Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba

hudondoza asali,

na maneno ya kinywa chake

ni laini kuliko mafuta;

lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,

mkali kama upanga ukatao kuwili.

Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;

hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.

Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima;

njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba

hudondoza asali,

na maneno ya kinywa chake

ni laini kuliko mafuta;

lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,

mkali kama upanga ukatao kuwili.

Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;

hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.

Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima;

njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

Sasa basi wanangu, nisikilizeni;

msiache ninalowaambia.

Njia zenu ziwe mbali naye,

msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine

na miaka yako kwa aliye mkatili,

Njia zenu ziwe mbali naye,

msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine

na miaka yako kwa aliye mkatili,

wageni wasije wakasherehekea utajiri wako

na jitihada yako ikatajirisha

nyumba ya mwanaume mwingine.

Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,

wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

Utasema, "Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!

Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

Sikuwatii walimu wangu

wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa

katikati ya kusanyiko lote."

Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri:

matiti yake na yakutosheleze siku zote,

nawe utekwe daima na upendo wake.

Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba?

Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?

Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo

na mapito yake kwenye roho za waliokufa.

Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi,

au kufikia mapito ya uzima.

Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;

yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana

atatumbukia ndani yake.

Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe.

Maisha Ya Kiroho

Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.

Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.

Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.

Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu.

Nimempa muda ili atubu kwa ajili ya uasherati wake, lakini hataki. Kwa hiyo nitamtupa kwenye kitanda cha mateso, na nitawafanya hao wanaozini naye kupata mateso makali wasipotubia njia zake.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-