O adultério
O adultério é pecado grave que destrói alianças, famílias e vidas. A Bíblia condena firmemente a infidelidade conjugal e chama à pureza, fidelidade e santidade no casamento.
A lei de Deus
Não adulterarás. Quem comete adultério destrói a própria alma. A Palavra de Deus é clara e direta sobre este pecado.
Usizini.
Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.
Maana wivu ni ghadhabu ya mtu;
Wala hatahurumia siku ya kujilipizia kisasi.
Hatakubali fidia yoyote;
Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
Je! Mtu aweza kuchukua moto kifuani pake,
Na nguo zake zisiteketezwe?
Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto,
Na nyayo zake zisiungue?
Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake;
Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
Jesus ensina
Quem olhar para uma mulher com intenção impura já adulterou no coração. Jesus elevou o padrão da pureza.
Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.
Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.
Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake kama hawa; nawe wasemaje? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi. Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika ardhi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. Yesu akainuka asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; wala usitende dhambi tena.]
Armadilhas e consequências
Os lábios da mulher estranha destilam mel, mas o seu fim é amargo. Fuja da imoralidade — o adultério escraviza.
Maana midomo ya malaya hudondosha asali,
Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;
Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.
Miguu yake inateremkia mauti;
Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;
Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari.
Maana midomo ya malaya hudondosha asali,
Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;
Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.
Miguu yake inateremkia mauti;
Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;
Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari.
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,
Wala msiache maneno ya kinywa changu.
Itenge njia yako mbali naye,
Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
Usije ukawapa wengine heshima yako,
Na wakatili miaka yako;
Itenge njia yako mbali naye,
Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
Usije ukawapa wengine heshima yako,
Na wakatili miaka yako;
Wageni wasije wakashiba nguvu zako;
Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,
Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo,
Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu,
Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!
Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote,
Katikati ya mkutano na kusanyiko.
Ni ayala apendaye na paa apendezaye;
Matiti yake yakutoshe sikuzote;
Na kwa upendo wake ushangilie daima.
Mwanangu! Mbona unashangilia malaya,
Na kukikumbatia kifua cha mgeni?
Maana nyumba yake inaelekea mauti,
Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.
Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja,
Wala hawazifikilii njia za uzima.
Kinywa cha malaya ni shimo refu;
Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;