Agradecimento pela vida
Agradecer pela vida é reconhecer que cada respiração é dom de Deus. Toda criatura que tem fôlego louve ao Senhor — porque Ele nos formou e nos sustenta com amor.
Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.
Msifuni Bwana!
Kumsifu Mungu Mwokozi
Msifuni Bwana! kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.
Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,
Nitamsifu Bwana maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu sifa
wakati wote niishipo.
Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.
Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu.
Umbile langu halikufichika kwako,
nilipoumbwa mahali pa siri.
Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,
macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.
Siku zangu zote ulizonipangia
ziliandikwa katika kitabu chako
kabla haijakuwepo hata moja.
Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote;
nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.
Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,
ninapofurahi katika Bwana.
Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Upendo wako usiokoma
ni wa thamani mno!
Watu wakuu na wadogo
hujificha uvulini wa mbawa zako.
Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako,
nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.
Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,
katika nuru yako twaona nuru.
Maombi Ya Shukrani
Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,
kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.
Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake
Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,
nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
Nitafurahi na kushangilia ndani yako.
Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Baraka Za Kiroho Katika Kristo Yesu
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo.
Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.
mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa, ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.
Ukuu Wa Kristo
Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni Bwana Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.
Ee Bwana, ulichukua shauri langu,
ukaukomboa uhai wangu.
Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,
makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.
Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,
Ee Bwana Mungu wangu.
"Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,
nilikukumbuka wewe, Bwana,
nayo maombi yangu yalikufikia wewe,
katika Hekalu lako takatifu.