Publicidade

Agradecimento

Por Bíblia Online

O agradecimento é a linguagem natural do cristão. Em tudo dai graças! A gratidão a Deus transforma a perspectiva, fortalece a fé e produz alegria em todos os tempos.

Dar graças sempre

Em tudo dai graças, porque esta é a vontade de Deus em Cristo Jesus para convosco. A gratidão é atitude fundamental.

shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.

Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.

Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru.

Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Louvor e gratidão

Entrai pelas portas com ação de graças. Rendei graças ao Senhor porque Ele é bom e a sua bondade dura para sempre.

Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

na katika nyua zake kwa kusifu,

mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.

Fadhili zake zadumu milele.

Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema,

upendo wake wadumu milele.

Tuje mbele zake kwa shukrani,

tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,

mfalme mkuu juu ya miungu yote.

Ni vyema kumshukuru Bwana

na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

kuutangaza upendo wako asubuhi,

na uaminifu wako wakati wa usiku,

Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi,

naye aiandaa njia yake

ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu."

Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,

wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru

na kulisifu Jina lako tukufu.

Expressões de gratidão

Graças a Deus pelo seu dom inefável! A gratidão se expressa em oração, louvor e generosidade para com os outros.

Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu.

Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote.

Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza.

Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake.

Utukufu ni wake milele! Amen.

" ‘ "Bwana akubariki

na kukulinda;

Bwana akuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

Bwana akugeuzie uso wake

na kukupa amani." ’

Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

nitakutolea dhabihu.

Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

Wokovu watoka kwa Bwana."

Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.

Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.

sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu.

Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji,

Wakati wote na kila mahali, kwa namna yoyote, mtukufu sana Feliksi, tumeyapokea mambo haya yote kwa shukrani nyingi.

Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.

Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

Yesu akauliza, "Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?" Yesu akamwambia, "Inuka na uende zako, imani yako imekuponya."

Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, wakapaza sauti, wakasema, "Yesu, Bwana, tuhurumie!"

Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.

Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

Yesu akauliza, "Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?" Yesu akamwambia, "Inuka na uende zako, imani yako imekuponya."

Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi.

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-