Ajuda
Deus é nosso auxílio e socorro em todo tempo. Ele não dorme nem cochila. O Senhor é nosso ajudador — não precisamos temer o que o homem possa nos fazer.
Msaada wangu hutoka kwa Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Hakika Mungu ni msaada wangu,
Bwana ndiye anayenitegemeza.
Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana,
yeye ni ngome yao wakati wa shida.
Bwana huwasaidia na kuwaokoa,
huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,
kwa maana wanamkimbilia.
Ee Bwana Mwokozi wangu,
uje upesi kunisaidia.
Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,
kwa ajili ya utukufu wa jina lako;
tuokoe na kutusamehe dhambi zetu
kwa ajili ya jina lako.
Bwana asifiwe,
kwa maana amesikia kilio changu
nikimwomba anihurumie.
Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,
moyo wangu umemtumaini yeye,
nami nimesaidiwa.
Moyo wangu unarukaruka kwa furaha
nami nitamshukuru kwa wimbo.
Kama Bwana asingelinisaidia upesi,
ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.
Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
nikushikaye mkono wako wa kuume
na kukuambia, Usiwe na hofu,
nitakusaidia.
Hunipa ngao yako ya ushindi,
unajishusha chini ili kuniinua.
"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.
Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa. Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
katika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.
Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.