Publicidade

Alma

Por Bíblia Online

A alma é a parte mais íntima do ser humano — sede da vida, dos afetos e do encontro com Deus. A Bíblia convida a cuidar da alma com zelo e a aquietá-la diante do Senhor.

A alma diante de Deus

Bendize ao Senhor, ó minha alma! A alma suspira por Deus como a corça suspira pelas águas — com sede de eternidade.

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Vyote vilivyomo ndani yangu

vilihimidi jina lake takatifu.

Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,

nakutafuta kwa moyo wote;

nafsi yangu inakuonea kiu,

mwili wangu unakuonea wewe shauku,

katika nchi kame na iliyochoka

mahali ambapo hapana maji.

Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?

Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

Weka tumaini lako kwa Mungu,

kwa sababu bado nitamsifu,

Mwokozi wangu na Mungu wangu.

Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko;

wokovu wangu watoka kwake.

Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,

katika neno lake naweka tumaini langu.

Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha

ninapokuimbia sifa,

mimi, ambaye umenikomboa.

Sheria ya Bwana ni kamilifu,

ikihuisha nafsi.

Shuhuda za Bwana ni za kuaminika,

zikimpa mjinga hekima.

Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo

na ndimi za udanganyifu.

Cuidar da alma

Que aproveita ao homem ganhar o mundo inteiro e perder a sua alma? Buscar a Deus de toda alma é o caminho da vida.

Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

Yesu akamjibu, " ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’

Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.

Lakini kama mtamtafuta Bwana Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote.

Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Mose mtumishi wa Bwana alizowapa: yaani kumpenda Bwana Mungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote."

"Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njema Bwana Mungu wenu alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia.

Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

"Simama kwenye njia panda utazame,

ulizia mapito ya zamani,

ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,

nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’

Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali,

ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-