Amigo
O amigo verdadeiro é dádiva rara de Deus. Ele ama em todo tempo, fala a verdade em amor, aconselha com sabedoria e permanece fiel nas adversidades da vida.
Amizade verdadeira
Há amigo mais chegado que um irmão. Em todo tempo ama o amigo. O perfume e o incenso alegram o coração — assim o conselho doce do amigo.
Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,
bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.
Rafiki hupenda wakati wote
naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.
Manukato na uvumba huleta furaha moyoni,
nao uzuri wa rafiki huchipuka
kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.
Kama vile chuma kinoavyo chuma,
ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
Afadhali karipio la wazi
kuliko upendo uliofichika.
Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu,
bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,
tena usiende nyumbani mwa ndugu yako
wakati umepatwa na maafa.
Bora jirani wa karibu
kuliko ndugu aliye mbali.
Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,
bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.
Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka,
usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,
la sivyo utajifunza njia zake
na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.
Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,
bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?
Mali huleta marafiki wengi,
bali rafiki wa mtu maskini humwacha.
Jesus, o amigo
Já não vos chamo servos, mas amigos. O maior amor é dar a vida pelo amigo. Jesus é o amigo que nunca falha.
Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu.
Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu. Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.
Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, "Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki," naye akaitwa rafiki wa Mungu.
Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.
Companheiros de fé
Dois são melhores do que um. Os companheiros de fé se fortalecem mutuamente e caminham juntos com o Senhor.
Wawili ni afadhali kuliko mmoja,
kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:
Kama mmoja akianguka,
mwenzake atamwinua.
Lakini ni jambo la kuhuzunisha
kwa mtu yule aangukaye
naye hana wa kumwinua!
Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza
wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.
Ni kama vile umande wa Hermoni
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake,
naam, hata uzima milele.
Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao,
kwa wote wanaofuata mausia yako.
Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe.
Msidanganyike: "Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema."