Pular para o conteúdo
Publicidade

Aniversário de criança

Por Bíblia Online

O aniversário de uma criança é momento de celebrar o presente precioso que Deus deu. Cada criança é formada e conhecida por Deus desde antes de nascer.

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,

Uliniunga tumboni mwa mama yangu.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa

Kwa njia ya ajabu ya kutisha.

Matendo yako ni ya ajabu,

Na nafsi yangu yajua sana,

Mifupa yangu haikusitirika kwako,

Nilipoumbwa kwa siri,

Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;

Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;

Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia,

Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

Mawazo yako ni mazito sana kwangu;

Ee Mungu; nayo ni makuu sana.

Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,

Tutashangilia na kuifurahia.

Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu,

Tujipatie moyo wa hekima.

Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,

Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,

Ninakusifu Wewe daima.

Neno moja nimelitaka kwa BWANA,

Nalo ndilo nitakalolitafuta,

Nikae nyumbani mwa BWANA

Siku zote za maisha yangu,

Niutazame uzuri wa BWANA,

Na kutafakari hekaluni mwake.

Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,

Ulinisalimisha matitini mwa mama yangu.

Kwako nilitupwa tangu tumboni,

Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.

Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba;

Maana nilikuwa mwana kwa baba yangu,

Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.

Naye akanifundisha, akaniambia,

Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;

Shika amri zangu ukaishi.

Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Seja o primeiro