Aniversário de idoso
O aniversário de um idoso é celebração de uma vida longa e cheia de experiências com Deus. A Bíblia honra os cabelos brancos como coroa de glória e prova da fidelidade divina.
Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema,
upendo wake wadumu milele.
Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,
tushangilie na kufurahi ndani yake.
Sifa Na Wema Wa Mungu
Nitamtukuza Bwana nyakati zote,
sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,
moyo wangu umemtumaini yeye,
nami nimesaidiwa.
Moyo wangu unarukaruka kwa furaha
nami nitamshukuru kwa wimbo.
Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa
kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.
Umenijulisha njia ya uzima;
utanijaza na furaha mbele zako,
pamoja na furaha za milele
katika mkono wako wa kuume.
Jambo moja ninamwomba Bwana,
hili ndilo ninalolitafuta:
niweze kukaa nyumbani mwa Bwana
siku zote za maisha yangu,
niutazame uzuri wa Bwana
na kumtafuta hekaluni mwake.
Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,
ili tujipatie moyo wa hekima.
Mvi ni taji ya utukufu;
hupatikana kwa maisha ya uadilifu.
Utukufu wa vijana ni nguvu zao,
mvi ni fahari ya uzee.
bali wale wamtumainio Bwana
atafanya upya nguvu zao.
Watapaa juu kwa mbawa kama tai;
watapiga mbio wala hawatachoka,
watatembea kwa miguu wala hawatazimia.
"Sasa basi, kama vile Bwana alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano! Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule.
" ‘ "Bwana akubariki
na kukulinda;
Bwana akuangazie nuru ya uso wake
na kukufadhili;
Bwana akugeuzie uso wake
na kukupa amani." ’
Gayo Anasifiwa Kwa Ajili Ya Ukarimu Wake
Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.