Pular para o conteúdo
Publicidade

Aniversário de idoso

Por Bíblia Online

O aniversário de um idoso é celebração de uma vida longa e cheia de experiências com Deus. A Bíblia honra os cabelos brancos como coroa de glória e prova da fidelidade divina.

Shukrani kwa kukombolewa katika dhiki

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,

Tutashangilia na kuifurahia.

Sifa kwa kukombolewa katika shida

Nitamhimidi BWANA kila wakati,

Sifa zake zi kinywani mwangu daima.

BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.

Moyo wangu umemtumaini,

Nami nimesaidiwa;

Basi, moyo wangu unashangilia,

Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

Umenitia furaha moyoni mwangu,

Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

Utanijulisha njia ya uzima;

Mbele za uso wako kuna furaha tele;

Na katika mkono wako wa kulia

Mna mema ya milele.

Neno moja nimelitaka kwa BWANA,

Nalo ndilo nitakalolitafuta,

Nikae nyumbani mwa BWANA

Siku zote za maisha yangu,

Niutazame uzuri wa BWANA,

Na kutafakari hekaluni mwake.

Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu,

Tujipatie moyo wa hekima.

Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu,

Kama kikionekana katika njia ya haki.

Fahari ya vijana ni nguvu zao,

Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.

bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Sasa basi, angalia, yeye BWANA ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arubaini na mitano, tangu wakati huo BWANA alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli walipokuwa wanapitia jangwani; na sasa tazama, hivi leo nimetimiza umri wa miaka themanini na mitano. Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kwenda na kurudi.

BWANA akubariki, na kukulinda;

BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;

BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.

Gayo apongezwa kwa ukarimu wake

Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Seja o primeiro