Publicidade

Bem

Por Bíblia Online

Fazer o bem é mandamento de Deus e expressão prática do amor cristão. A Bíblia convida a praticar o bem a todos, com alegria, sem se cansar — porque colheremos no tempo próprio.

Uache mabaya ukatende mema,

Utafute amani ukaifuatie.

Umtumaini BWANA ukatende mema,

Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.

Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA

Katika nchi ya walio hai.

Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako,

Maana zimekuwako tokea zamani.

Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,

Wala maasi yangu.

Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,

Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.

BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote,

Na mwenye huruma katika matendo yake yote.

Ndipo utakapofahamu haki na hukumu,

Na adili, na kila njia njema.

Haja ya mwanadamu ni hisani yake;

Ni afadhali maskini kuliko mwongo.

Tunda la Roho

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Sifa za Mkristo

Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema.

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu

Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.

Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.

Naam, na kwa sababu iyo hiyo jitahidini sana ili katika imani yenu mtie na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu subira, na katika subira yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?

BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.

BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.

Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-