Bom dia
Cada manhã é presente de Deus. As misericórdias do Senhor se renovam cada dia. A Bíblia convida a começar o dia com louvor, oração e gratidão ao Criador.
Manhã com Deus
De manhã te apresentarei a minha oração. Pela manhã ouvirás a minha voz — eu te busco ao despertar.
Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana;
asubuhi naleta haja zangu mbele zako,
na kusubiri kwa matumaini.
Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie;
asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
Amka, nafsi yangu!
Amka, kinubi na zeze!
Nitayaamsha mapambazuko.
Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,
asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;
kwa maana wewe ndiwe ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa shida.
Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,
asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;
kwa maana wewe ndiwe ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa shida.
Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.
Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,
Mungu unipendaye.
Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,
kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.
Nionyeshe njia nitakayoiendea,
kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu.
Na mimi katika haki nitauona uso wako,
niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.
Misericórdias renovadas
As misericórdias do Senhor se renovam cada manhã. Este é o dia que o Senhor fez — alegremo-nos e nos regozijemos nele.
Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
Nimeiambia nafsi yangu, "Bwana ni fungu langu,
kwa hiyo nitamngojea."
Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,
tushangilie na kufurahi ndani yake.
Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;
lisifuni jina lake takatifu.
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,
bali upendo wake hudumu siku zote.
Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,
lakini asubuhi kukawa na furaha.
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,
bali upendo wake hudumu siku zote.
Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,
lakini asubuhi kukawa na furaha.
Wale wanaoishi mbali sana
wanaogopa maajabu yako,
kule asubuhi ipambazukiapo
na kule jioni inakofifilia
umeziita nyimbo za furaha.
Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma,
ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.
Louvor matinal
Saciai-nos de manhã com a tua benignidade. Todo dia te louvarei e celebrarei o teu nome para sempre.
Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme,
nitalisifu jina lako milele na milele.
Kila siku nitakusifu
na kulitukuza jina lako milele na milele.
Ni vyema kumshukuru Bwana
na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
kuutangaza upendo wako asubuhi,
na uaminifu wako wakati wa usiku,
Mwimbieni Bwana wimbo mpya;
mwimbieni Bwana dunia yote.
Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake;
tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,
matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.
Ninaitafakari mchana kutwa.
Mchana Bwana huelekeza upendo wake,
usiku wimbo wake uko nami:
maombi kwa Mungu wa uzima wangu.
Ee Bwana, uturehemu,
tunakutamani.
Uwe nguvu yetu kila asubuhi
na wokovu wetu wakati wa taabu.
Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa,
ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka.
Huniamsha asubuhi kwa asubuhi,
huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.
Graça para o novo dia
O Senhor te abençoe e te guarde. Cada novo dia é oportunidade de viver sob a graça do Deus que nos ama.
" ‘ "Bwana akubariki
na kukulinda;
Bwana akuangazie nuru ya uso wake
na kukufadhili;
Bwana akugeuzie uso wake
na kukupa amani." ’
Panda mbegu yako asubuhi,
nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee,
kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa,
kwamba ni hii au ni ile,
au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.
Yeye huamka kungali bado giza
huwapa jamaa yake chakula
na mafungu kwa watumishi wake wa kike.
Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,
uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. Mungu akaiita nuru "mchana," na giza akaliita "usiku." Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyongʼaa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu.
Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye.