Publicidade

Casa de Deus

Por Bíblia Online

A casa de Deus é lugar de adoração, refúgio e encontro com o Sagrado. A Bíblia exalta o tabernáculo, o templo e a igreja como morada do Altíssimo entre seu povo.

A presença de Deus

Quão amáveis são os teus tabernáculos! Uma coisa pedi ao Senhor: habitar na casa do Senhor todos os dias da minha vida.

Siku moja katika nyua zako ni bora

kuliko siku elfu mahali pengine;

afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu

kuliko kukaa katika mahema ya waovu.

Jambo moja ninamwomba Bwana,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Bwana

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Bwana

na kumtafuta hekaluni mwake.

Heri wale uliowachagua

na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako!

Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako,

mema ya Hekalu lako takatifu.

Sifa Kwa Yerusalemu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,

"Twende nyumbani ya Bwana."

Hakika wema na upendo vitanifuata

siku zote za maisha yangu,

nami nitakaa nyumbani mwa Bwana

milele.

Neema Ya Mungu

Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni

unaostawi katika nyumba ya Mungu,

nautegemea upendo wa Mungu usiokoma

milele na milele.

Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila,

matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.

O templo

Minha casa será chamada casa de oração. O zelo da tua casa me consumiu. O verdadeiro templo é o corpo do cristão.

Yesu Atakasa Hekalu

Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. Akawaambia, "Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi."

Ilipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ngʼombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha. Akatengeneza mjeledi kutokana na kamba, akawafukuza wote kutoka kwenye eneo la Hekalu, pamoja na kondoo na ngʼombe. Akazipindua meza za wale wabadili fedha na kuzimwaga fedha zao. Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, "Waondoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa biashara?"

Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa imeandikwa: "Wivu wa nyumba yako utanila."

Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe,

kama nikikawia, utajua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ndiyo kanisa la Mungu aliye hai, lililo nguzo na msingi wa kweli.

Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mungu. Sisi ndio nyumba yake, kama tutashikilia sana ujasiri wetu na tumaini tunalojivunia.

"Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Mose, kulingana na kielelezo alichoona. Baba zetu wakiisha kulipokea hema kwa kupokezana wakiongozwa na Yoshua katika milki ya nchi kutoka kwa yale mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao, nalo likadumu katika nchi mpaka wakati wa Daudi, ambaye alipata kibali kwa Mungu, naye akaomba kwamba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. Lakini alikuwa Solomoni ndiye alimjengea Mungu nyumba.

"Hata hivyo, Yeye Aliye Juu Sana hakai kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kama nabii alivyosema:

" Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Mtanijengea nyumba ya namna gani?

asema Bwana.

Au mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote?

Hukumu Na Matumaini

Hili ndilo asemalo Bwana,

"Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?

Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?"

asema Bwana.

"Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, "Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua." Kwa hiyo akaogopa, akasema, "Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni."

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-