Publicidade

Compaixão

Por Bíblia Online

A compaixão é o coração de Deus em ação. Ele é compassivo e misericordioso, tardio em irar-se e grande em amor. Somos chamados a refletir essa compaixão no mundo.

Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,

ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;

Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,

si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.

Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,

midomo yangu itakuadhimisha.

Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,

kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

Ni mpya kila asubuhi,

uaminifu wako ni mkuu.

"Je, mama aweza kumsahau mtoto

aliyeko matitini mwake akinyonya,

wala asiwe na huruma

juu ya mtoto aliyemzaa?

Ingawa anaweza kusahau,

mimi sitakusahau wewe!

Tazama, nimekuchora kama muhuri

katika vitanga vya mikono yangu,

kuta zako zi mbele yangu daima.

Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

Ni nani Mungu kama wewe,

ambaye anaachilia dhambi

na kusamehe makosa

ya mabaki ya urithi wake?

Wewe huwi na hasira milele,

bali unafurahia kuonyesha rehema.

"Nitaiimarisha nyumba ya Yuda

na kuiokoa nyumba ya Yosefu.

Nitawarejesha kwa sababu

nina huruma juu yao.

Watakuwa kama watu ambao

sijawahi kuwakataa

kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wao,

nami nitawajibu.

"Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.

Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.

Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Kuteseka Kwa Kutenda Mema

Hatimaye, ninyi nyote kuweni na nia moja, wenye kuhurumiana, mkipendana kama ndugu, na mwe wasikitivu na wanyenyekevu.

Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo?

Mungu Wa Faraja Yote

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.

Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo: lakini yeye hakutenda dhambi.

Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.

Salamu Za Mwisho

Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-