Confiabilidade
A confiabilidade de Deus é absoluta. Ele é fiel em todas as suas promessas, constante em seu amor e seguro em seu caráter. Podemos confiar nele completamente.
Deus é fiel
O Senhor é fiel em todas as suas palavras e bondoso em todos os seus atos. Grande é a sua fidelidade!
Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
Bwana atatimiza kusudi lake kwangu,
Ee Bwana, upendo wako wadumu milele:
usiziache kazi za mikono yako.
Lakini kutoka milele hata milele
upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
kwa wale walishikao agano lake
na kukumbuka kuyatii mausia yake.
Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao,
kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,
Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki
naye hatawaacha waaminifu wake.
Watalindwa milele,
lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.
Lakini Bwana ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu.
Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.
Basi ujue kwamba Bwana Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake.
Bwana mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."
Caráter de Deus
Toda boa dádiva vem do alto. O Senhor é bom e sua misericórdia dura para sempre. Nele podemos descansar.
Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;
upendo wake wadumu milele.
Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe,
umejaa upendo kwa wote wakuitao.
kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu,
na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.
Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,
asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;
kwa maana wewe ndiwe ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa shida.
Mtwike Bwana fadhaa zako,
naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Hatauacha mguu wako uteleze,
yeye akulindaye hatasinzia,
Integridade e confiança
Eu sou o Alfa e o Ômega — Deus é o mesmo ontem, hoje e sempre. Fiel em o que realizou e realizará por cada filho.
"Mimi ni Alfa na Omega," asema Bwana Mungu, "aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi."
Wewe, Ee Bwana unatawala milele,
kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.
Ee Bwana, wewe ni Mungu wangu,
nitakutukuza na kulisifu jina lako,
kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu
umetenda mambo ya ajabu,
mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.
Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,
afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.
Masengenyo husaliti tumaini,
bali mtu mwaminifu hutunza siri.
Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
"Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.