Consolo
O consolo de Deus é bálsamo para a alma ferida. Ele nos conforta em todas as tribulações para que possamos consolar outros com o mesmo consolo divino.
Deus consola
Ainda que eu ande pelo vale da sombra da morte, não temerei mal algum. O Senhor consola, guia e está sempre presente.
Hata kama nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
nimhofu nani?
Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:
Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,
sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,
kwa yule ambaye humtafuta;
Confiança na aflição
Eu sei que o meu Redentor vive. Deus é força e escudo — mesmo na tribulação, Ele nos sustenta e consola.
Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai,
naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,
bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;
Hakika Mungu ni wokovu wangu;
nitamtumaini wala sitaogopa.
Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu."
Bwana mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako."
Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,
"Bwana ni msaada wangu; sitaogopa.
Mwanadamu anaweza kunitenda nini?"
Heri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.
Lakini mimi, namtazama Bwana kwa matumaini,
namngoja Mungu Mwokozi wangu;
Mungu wangu atanisikia mimi.
Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu.