Publicidade

Coração puro

Por Bíblia Online

Bem-aventurados os puros de coração, porque verão a Deus. A pureza de coração é alvo, privilégio e busca constante do cristão que deseja contemplar a face do Senhor.

Coração puro

Bem-aventurados os puros de coração. A pureza interior precede toda transformação externa e abre os olhos para ver a Deus.

Heri walio na moyo safi,

maana hao watamwona Mungu.

Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana?

Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,

yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake

au kuapa kwa kitu cha uongo.

Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana,

na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu,

na uufute uovu wangu wote.

Ee Mungu, uniumbie moyo safi,

uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.

Usinitupe kutoka mbele zako

wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.

Haki Ya Mungu
Zaburi ya Asafu.

Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,

kwa wale ambao mioyo yao ni safi.

Purificar-se

Todo o que tem essa esperança em Cristo se purifica. O amor procede de coração puro, boa consciência e fé sincera.

Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.

Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.

Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli.

Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo, mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu.

Fanyeni mambo yote bila kunungʼunika wala kushindana, ili msiwe na lawama wala hatia, bali mwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika kizazi chenye ukaidi na kilichopotoka, ambacho ndani yake ninyi mnangʼaa kama mianga ulimwenguni. Mkilishika neno la uzima, ili nipate kuona fahari siku ya Kristo kwamba sikupiga mbio wala kujitaabisha bure.

Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.

Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,

bali makusudi hupimwa na Bwana.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-