Crianças
As crianças ocupam lugar especial no coração de Deus. A Bíblia instrui a educá-las, protegê-las e ensiná-las nos caminhos do Senhor desde cedo — formando gerações que temem a Deus.
Herança do Senhor
Os filhos são herança do Senhor. Eles são presentes de Deus — cada criança é um milagre e uma responsabilidade sagrada.
Wana ni urithi utokao kwa Bwana,
watoto ni zawadi kutoka kwake.
Kisha wana wetu wakati wa ujana wao
watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,
binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa
kurembesha jumba la kifalme.
Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.
Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu.
Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
Njooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Bwana.
Instruir as crianças
Instrui a criança no caminho em que deve andar. A educação cristã é mandamento repetido através de toda a Escritura.
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.
Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,
bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.
Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,
bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.
Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,
bali yeye ampendaye
huwa mwangalifu kumwadibisha.
Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,
bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,
kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako
na kukuletea mafanikio.
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,
kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,
kama vile baba afanyavyo
kwa mwana apendezwaye naye.
baba alinifundisha akisema,
"Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;
yashike maagizo yangu na wewe utaishi.
Pata hekima, pata ufahamu;
usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.
Disciplinar com amor
A vara e a repreensão dão sabedoria. A disciplina produz o fruto pacífico da justiça nos que são exercitados por ela.
Fimbo ya maonyo hutia hekima,
bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo
humwaibisha mama yake.
Usimnyime mtoto adhabu,
ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa.
Msikilize baba yako, aliyekuzaa,
wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.
Nunua kweli wala usiiuze,
pata hekima, adabu na ufahamu.
Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake
ni mwana aletaye aibu na fedheha.
Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,
kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.
Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,
wamebarikiwa watoto wake baada yake.
Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,
kama tabia yake ni safi na adili.
Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake
na uchungu kwa yeye aliyemzaa.
Wana wa wana ni taji la wazee,
nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
Wana wa wana ni taji la wazee,
nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake,
bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.
Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu,
bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.
Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,
na mkufu wa kuipamba shingo yako.
"Basi sasa wanangu, nisikilizeni;
heri wale wanaozishika njia zangu.
Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima;
msiyapuuze.
Obediência e promessa
Filhos, obedecei a vossos pais no Senhor. Honra a teu pai e tua mãe para que viva muito tempo sobre a terra.
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, "upate baraka na uishi siku nyingi duniani."
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.
Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao,
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
Mshike amri na maagizo yake ninayowapa leo, ili mpate kufanikiwa ninyi na watoto wenu baada yenu, na mpate kuishi maisha marefu katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu siku zote.
Mwe waangalifu kutii masharti haya yote ninayowapa, ili kwamba siku zote mweze kufanikiwa, ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo jema na sahihi mbele za macho ya Bwana Mungu wenu.
akawaambia, "Yawekeni moyoni maneno yote ambayo nimewatangazia kwa makini siku hii ya leo, ili kwamba mpate kuwaagiza watoto wenu wayatii kwa bidii maneno yote ya sheria hii. Siyo maneno matupu tu kwenu, bali ni uzima wenu. Kwa hayo mtaishi maisha marefu katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki."
Crianças e o reino
Deixai vir a mim as crianças. Jesus honrou as crianças como modelo de fé e humildade para todo o seu povo.
Yesu akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa."
Yesu akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa."
Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, "Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?"
Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.
Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.
"Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.
"Angalia ili usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [
Wakati huo Yesu alisema, "Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo.
Heri walio wapatanishi,
maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea. Yesu alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa.
Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, "Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma."
Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Walipokwisha kula, Yesu akamuuliza Simoni Petro, "Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?"
Yeye akamjibu, "Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda."
Yesu akamwambia, "Lisha wana-kondoo wangu."
Identidade e crescimento
Somos filhos de Deus pelo Espírito de adoção. Crescer em Cristo é amadurecer em fé, obediência e amor ao próximo.
Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu.
Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, "Abba, yaani, Baba,"
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu watoto wa Mungu.
Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu.
Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo.
Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.
Nawaandikia ninyi, watoto wadogo,
kwa sababu dhambi zenu
zimesamehewa kwa ajili ya Jina lake.
Watoto wapendwa, jilindeni nafsi zenu kutokana na sanamu. Amen.
Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia.
Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.
Nanyi mmesahau yale maneno ya kuwaonya yanayowataja ninyi kuwa wana, yakisema:
"Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana,
wala usikate tamaa akikukemea,
kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,
na humwadhibu kila mmoja
anayemkubali kuwa mwana."
Vumilieni taabu kwa ajili ya kufunzwa adabu. Mungu anawatendea ninyi kama watoto wake, kwa maana ni mtoto yupi asiyeadibishwa na mzazi wake? Kama hakuna kuadibishwa (ambalo ni fungu la watoto wote), basi ninyi ni watoto wa haramu wala si watoto halali. Tena, sisi sote tunao baba wa kimwili, waliotuadibisha nasi tukawaheshimu kwa ajili ya hilo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa Baba wa roho zetu ili tuishi?
Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.
Wakamjibu, "Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako."
Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vilevile.
Transmitir a fé
Contaremos à geração vindoura os louvores do Senhor. O legado de fé é o maior presente que damos aos nossos filhos.
Watoto wako wote watafundishwa na Bwana,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
Watoto wako wote watafundishwa na Bwana,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,
kama ninavyofanya leo.
Baba huwaambia watoto wao
habari za uaminifu wako.
"Je, mama aweza kumsahau mtoto
aliyeko matitini mwake akinyonya,
wala asiwe na huruma
juu ya mtoto aliyemzaa?
Ingawa anaweza kusahau,
mimi sitakusahau wewe!
Tazama, nimekuchora kama muhuri
katika vitanga vya mikono yangu,
kuta zako zi mbele yangu daima.
Baada ya kuona hali ilivyo, nikasimama na kuwaambia wakuu, maafisa na wengine wote, "Msiwaogope. Mkumbukeni Bwana, ambaye ni mkuu mwenye kuogofya. Piganeni kwa ajili ya ndugu zenu, wana wenu na binti zenu, wake zenu na nyumba zenu."
Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi.
Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.
Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.
Hatutayaficha kwa watoto wao;
tutakiambia kizazi kijacho
matendo yastahiliyo sifa ya Bwana,
uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.
Aliagiza amri kwa Yakobo
na akaweka sheria katika Israeli,
ambazo aliwaamuru baba zetu
wawafundishe watoto wao,
ili kizazi kijacho kizijue,
pamoja na watoto ambao watazaliwa,
nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.
Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu,
nao wasingesahau matendo yake,
bali wangalizishika amri zake.