Publicidade

Tomar uma decisão

Por Bíblia Online

Tomar decisões com sabedoria é um dos maiores desafios da vida. A Bíblia nos ensina a buscar a Deus em oração, na Palavra e no conselho, confiando que Ele dirige os nossos passos.

Buscar a Deus

Se algum de vós tem falta de sabedoria, peça a Deus. Ele dá generosamente e sem repreensão a todos os que pedem.

Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.

Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Bwana, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

Conselho e direção

Onde não há conselho os planos se frustam. Toda Escritura é útil para nos guiar nas decisões da vida.

Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka,

bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.

Kura hupigwa kwa siri,

lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.

Mtu ajitengaye na wengine

hufuata matakwa yake mwenyewe;

hupiga vita kila shauri jema.

Mpumbavu hafurahii ufahamu,

bali hufurahia kutangaza

maoni yake mwenyewe.

Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia,

pamoja na aibu huja lawama.

Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji,

bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.

Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,

au kumnyima haki asiye na hatia.

Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi

na kinywa chake hualika kipigo.

Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake

na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;

huingia sehemu za ndani sana za mtu.

Mtu aliye mlegevu katika kazi yake

ni ndugu na yule anayeharibu.

Jina la Bwana ni ngome imara,

wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,

wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.

Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,

bali unyenyekevu hutangulia heshima.

Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza,

huo ni upumbavu wake na aibu yake.

Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa

bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?

Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki,

ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.

Walipofika mpaka wa Misia, wakajaribu kuingia Bithinia lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu.

Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli. Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, "Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia." Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao.

Confiar e seguir

Seja o que for que façais, fazei tudo para a glória de Deus. O sábio ouve a Deus antes de agir.

Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Kwa sababu hii, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, basi na tuweke kando kila kitu kinachotuzuia na ile dhambi inayotuzinga kwa urahisi, nasi tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa kwa ajili yetu.

Bwana akamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, "Omba lolote utakalo nikupe."

Solomoni akajibu, "Umemfanyia mtumishi wako, baba yangu Daudi, fadhili nyingi, kwa kuwa alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki, tena mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii kuu kwani umempa mwana wa kuketi kwenye kiti chake cha ufalme, kama ilivyo leo.

"Sasa, Ee Bwana Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme badala ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu, wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu. Mtumishi wako yuko hapa miongoni mwa watu uliowachagua: taifa kubwa, watu wengi wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao. Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu ili kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana, ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi hivi?"

Bwana akapendezwa kwamba Solomoni ameliomba jambo hili. Basi Mungu akamwambia, "Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki, nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako.

Mke wake akamwambia, "Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!"

Akamjibu, "Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?"

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-