Dependência
A dependência de Deus é o caminho da verdadeira liberdade. Sem Cristo, nada podemos fazer. Mas em Deus encontramos sustento, direção e força para todo desafio.
Sem Ele nada podemos
Sem mim nada podeis fazer. O cristão que se desconecta da videira seca — mas o que permanece dá muito fruto.
"Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.
Ee Mungu, uniweke salama,
kwa maana kwako nimekimbilia.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima.
Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.
Bwana asipoijenga nyumba,
wajengao hufanya kazi bure.
Bwana asipoulinda mji,
walinzi wakesha bure.
Sio kwa upanga wao waliipata nchi,
wala si mkono wao uliwapatia ushindi;
ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,
na nuru ya uso wako,
kwa kuwa uliwapenda.
Bwana atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu."
Depender do Senhor
Confia no Senhor de todo o coração e não te estribes no teu próprio entendimento. Em todos os caminhos o reconhece.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
katika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.
Moyo wa mtu huifikiri njia yake,
bali Bwana huelekeza hatua zake.
Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,
lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.
Baraka ya Bwana hutajirisha,
wala haichanganyi huzuni.
Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,
bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu
na fungu langu milele.
Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.
Nayainua macho yangu nitazame vilima,
msaada wangu utatoka wapi?
Msaada wangu hutoka kwa Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.
Hatauacha mguu wako uteleze,
yeye akulindaye hatasinzia,
Niliposema, "Mguu wangu unateleza,"
Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.
Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana,
naye akanijibu kwa kuniweka huru.
Bwana ndiye mchungaji wangu,
sitapungukiwa na kitu.
Hunilaza katika malisho
ya majani mabichi,
kando ya maji matulivu huniongoza,
Contentamento e confiança
Aprendi a viver contente em toda situação. A dependência de Deus nos livra da ansiedade e nos firma na paz.
Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote.
Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
nikushikaye mkono wako wa kuume
na kukuambia, Usiwe na hofu,
nitakusaidia.
Huwapa nguvu waliolegea
na huongeza nguvu za wadhaifu.
Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu.
Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu.
Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.
"Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako.