Deus
Deus é a realidade suprema do universo — o criador, sustentador e redentor de tudo o que existe. Conhecê-lo é a essência da vida eterna e o maior privilégio da existência humana.
Quem é Deus
Não há santo como o Senhor. Tu és grande e fazes maravilhas — só tu és Deus. Sua majestade transcende toda compreensão.
"Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Bwana,
hakuna mwingine zaidi yako;
hakuna Mwamba kama Mungu wetu.
"Tazama jinsi ulivyo mkuu, Ee Bwana Mwenyezi! Hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe,
Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini Mungu ni mjenzi wa kila kitu.
Ee Bwana, wewe ni Mungu wangu,
nitakutukuza na kulisifu jina lako,
kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu
umetenda mambo ya ajabu,
mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.
"Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,
wala njia zenu si njia zangu,"
asema Bwana.
Deus é amor
Deus é amor. Quem permanece no amor permanece em Deus e Deus nele. Nós amamos porque Ele nos amou primeiro.
Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.
Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.
Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.
Ikiwa mtu atasema, "Nampenda Mungu," lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona?
Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Bwana Mungu wako yu pamoja nawe,
yeye ni mwenye nguvu kuokoa.
Atakufurahia kwa furaha kubwa,
atakutuliza kwa pendo lake,
atakufurahia kwa kuimba."
Buscar a Deus
Buscareis o Senhor e o encontrareis quando o buscardes de todo o coração. Provai e vede que o Senhor é bom.
Lakini kama mtamtafuta Bwana Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote.
Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.
Nilimwambia Bwana, "Wewe ndiwe Bwana wangu;
pasipo wewe sina jambo jema."
Nani niliye naye mbinguni ila wewe?
Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.
Wakati ninapoogopa,
nitakutumaini wewe.
Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,
uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.
Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima
na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana.
Viver com Deus
Sê forte e corajoso, porque o Senhor teu Deus é contigo. Em Deus encontramos a razão de existir.
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako."
Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini!
"Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja
na utukufu wa Bwana umezuka juu yako.
Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
nikushikaye mkono wako wa kuume
na kukuambia, Usiwe na hofu,
nitakusaidia.
Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.