Pular para o conteúdo
Publicidade

Dia das crianças

Por Bíblia Online

As crianças são preciosas aos olhos de Deus. Jesus as acolheu, abençoou e ensinou que delas é o Reino dos Céus — modelos de fé, pureza e humildade.

Jesus e as crianças

Deixai vir a mim as crianças. Jesus abraçou, abençoou e honrou as crianças como modelo de fé para os adultos.

Yesu akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa."

Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni

Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, "Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?"

Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.

Mfano Wa Kondoo Aliyepotea

"Angalia ili usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [

Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, "Hosana Mwana wa Daudi," walikasirika.

Wakamuuliza Yesu, "Je, unasikia hayo hawa wanayosema?"

Akawajibu, "Naam; kwani hamkusoma,

" Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao

umeamuru sifa?"

Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe." Akawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.

Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, "Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma."

Instruir e proteger

Instrui a criança no caminho de Deus. Elas são herança do Senhor — presentes sagrados que devemos educar com amor.

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,

naye hataiacha hata akiwa mzee.

Watoto wako wote watafundishwa na Bwana,

nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.

Wana ni urithi utokao kwa Bwana,

watoto ni zawadi kutoka kwake.

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, "upate baraka na uishi siku nyingi duniani."

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

" ‘ "Bwana akubariki

na kukulinda;

Bwana akuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

Bwana akugeuzie uso wake

na kukupa amani." 

Seja o primeiro