Publicidade

Dia dos pais

Por Bíblia Online

O Dia dos Pais celebra o amor e o sacrifício paterno. A Bíblia honra os pais como provedores, protetores e guias espirituais que moldam as próximas gerações.

O pai que educa

Instrui a criança no caminho em que deve andar. O pai justo educa com amor, firmeza e o exemplo de uma vida íntegra.

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,

naye hataiacha hata akiwa mzee.

Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,

bali yeye ampendaye

huwa mwangalifu kumwadibisha.

Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,

wamebarikiwa watoto wake baada yake.

Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,

naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

Yeye amchaye Bwana ana ngome salama,

na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.

Honra e alegria

Honra a teu pai e tua mãe. Os filhos são herança do Senhor, e a família que serve a Deus junta é inabalável.

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

Wana ni urithi utokao kwa Bwana,

watoto ni zawadi kutoka kwake.

Kama mishale mikononi mwa shujaa

ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

Heri mtu ambaye podo lake

limejazwa nao.

Hawataaibishwa wanaposhindana

na adui zao langoni.

Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana."

Maneno Ya Mwisho

Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, kuweni mashujaa kuweni hodari.

Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake.

"Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.

"Yule mwana akamwambia baba yake, Baba, nimekosa mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.

"Lakini baba yake akawaambia watumishi, Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake. Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-