Dinheiro
O dinheiro é ferramenta que pode ser usada para o bem ou para o mal. A Bíblia nos ensina a administrar recursos com sabedoria, generosidade e temor ao Senhor.
Perspectiva bíblica
Guardai-vos da avareza. A vida não consiste na abundância de bens. O dinheiro é servo, nunca senhor.
Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako pia.
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu?
Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa,
Kama tai arukaye mbinguni.
Usijitaabishe ili kupata utajiri;
Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.
Apendaye fedha hatashiba fedha,
Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza.
Hayo pia ni ubatili.
Administrar com sabedoria
Honra ao Senhor com as tuas primícias. O sábio administra seus recursos com prudência e visão de eternidade.
Mheshimu BWANA kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Baraka ya BWANA hutajirisha,
Wala hachanganyi huzuni nayo.
Hazina za uovu hazifaidii kitu;
Bali haki huokoa na mauti.
Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;
Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu?
Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha.
Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi;
Na neema kuliko fedha na dhahabu.
Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA;
Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.
Haja ya mwanadamu ni hisani yake;
Ni afadhali maskini kuliko mwongo.
Uniondolee ubatili na uongo;
Usinipe umaskini wala utajiri;
Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
Perigos e armadilhas
Quem quer enriquecer cai em tentação. Fuja do amor ao dinheiro e busque contentamento no Senhor.
Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu.
Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.
Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu;
Bali haki huokoa na mauti.
Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;
Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.
Tudo vem de Deus
De ti vem tudo, e das tuas mãos to damos. Os tributos são devidos — dai a César o que é de César e a Deus o que é de Deus.
Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Kwa sababu hiyo tena mnalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.
Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora
Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
Maana mikono ya wasio haki itavunjika,
Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
Nimeifurahia njia ya shuhuda zako
Kana kwamba ni mali mengi.