Ensinar
Ensinar é mandamento e dom. A Bíblia exorta pais, líderes e mestres a transmitir a verdade divina com fidelidade, paciência e sabedoria para as próximas gerações.
Ensinar a Palavra
Toda Escritura é útil para ensinar. Quem ouve as palavras de Jesus e as pratica é como o homem sábio que construiu sobre a rocha.
Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.
"Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.
Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.
Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:
Kwa kupata hekima na nidhamu;
kwa kufahamu maneno ya busara;
kwa kujipatia nidhamu na busara,
kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
huwapa busara wajinga,
maarifa na akili kwa vijana;
wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,
wenye kupambanua na wapate mwongozo;
kwa kufahamu mithali na mifano,
misemo na vitendawili vya wenye hekima.
Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Instruir as gerações
Ensina a criança nos caminhos de Deus. A geração que não conhece o Senhor perde a herança espiritual da fé.
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,
na mkufu wa kuipamba shingo yako.
Mwanangu, zishike amri za baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
Yafunge katika moyo wako daima,
yakaze kuizunguka shingo yako.
Wakati utembeapo, yatakuongoza;
wakati ulalapo, yatakulinda;
wakati uamkapo, yatazungumza nawe.
Kwa maana amri hizi ni taa,
mafundisho haya ni mwanga
na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,
Pata hekima, pata ufahamu;
usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.
Usimwache hekima naye atakuweka salama;
mpende, naye atakulinda.
Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.
Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
Mstahi, naye atakukweza;
mkumbatie, naye atakuheshimu.
Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
mshike, maana yeye ni uzima wako.
Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu
wala usitembee katika njia ya watu wabaya.
Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Epusha kinywa chako na ukaidi;
weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako.
Macho yako na yatazame mbele,
kaza macho yako moja kwa moja mbele yako.
Sawazisha mapito ya miguu yako
na njia zako zote ziwe zimethibitika.
Usigeuke kulia wala kushoto;
epusha mguu wako na ubaya.
Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
"Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu,
sikilizeni maneno ya kinywa changu.
Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo,
nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:
yale ambayo tuliyasikia na kuyajua,
yale ambayo baba zetu walituambia.
Hatutayaficha kwa watoto wao;
tutakiambia kizazi kijacho
matendo yastahiliyo sifa ya Bwana,
uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.
Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua Bwana, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli.
Fidelidade no ensino
Quem ensina com fidelidade merece dupla honra. Cuidado com doutrinas falsas — permaneçam na doutrina de Cristo.
Wazee wa kanisa wanaoongoza shughuli za kanisa vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha. Kwa maana Maandiko husema, "Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka," tena, "Mfanyakazi anastahili mshahara wake."
Jiepushe na maneno mabaya, yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa heshima kwa Mungu. Mafundisho yao yataenea kama kidonda kisichopona. Miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto
Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia.
Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha. Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, "Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?"
Ndipo Yesu akawajibu, "Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma. Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe. Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake.