Ensinar
Ensinar é mandamento e dom. A Bíblia exorta pais, líderes e mestres a transmitir a verdade divina com fidelidade, paciência e sabedoria para as próximas gerações.
Ensinar a Palavra
Toda Escritura é útil para ensinar. Quem ouve as palavras de Jesus e as pratica é como o homem sábio que construiu sobre a rocha.
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Instruir as gerações
Ensina a criança nos caminhos de Deus. A geração que não conhece o Senhor perde a herança espiritual da fé.
Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako,
Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,
Na mikufu shingoni mwako.
Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako.
Yafunge hayo katika moyo wako daima;
Jivike hayo shingoni mwako.
Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda,
Na uamkapo yatazungumza nawe.
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru,
Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;
Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
Usimwache, naye atakusitiri;
Umpende, naye atakulinda.
Bora hekima, basi jipatie hekima;
Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Umtukuze, naye atakukuza;
Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
Mshike, maana yeye ni uzima wako.
Usiingie katika njia ya waovu,
Wala usitembee katika njia ya wabaya.
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Jiepushe na kinywa cha ujeuri,
Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
Macho yako yatazame mbele,
Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
Ulisawazishe pito la mguu wako,
Na njia zako zote zithibitike;
Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto;
Ondoa mguu wako maovuni.
Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima,
Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;
Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,
Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
Nitafumbua kinywa changu kwa mithali,
Niyatamke mafumbo ya kale.
Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu,
Ambayo baba zetu walituambia.
Hayo hatutawaficha wana wao,
Huku tukiwaambia kizazi kingine,
Sifa za BWANA, na nguvu zake,
Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.
Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
Fidelidade no ensino
Quem ensina com fidelidade merece dupla honra. Cuidado com doutrinas falsas — permaneçam na doutrina de Cristo.
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kutoa unabii na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.
Jiepushe na maneno machafu yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu, na neno lao litaenea kama donda ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alipanda kuingia hekaluni, akafundisha. Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenituma. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyemtuma, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.