Publicidade

Esperar no Senhor

Por Bíblia Online

Esperar no Senhor é ato de fé e confiança. A Bíblia promete que os que esperam em Deus renovam as forças, recebem direção e experimentam a fidelidade divina no tempo certo.

Renovar as forças

Os que esperam no Senhor renovam as forças. Sobem como águias, correm e não se cansam, caminham e não se fatigam.

bali wale wamtumainio Bwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

Mngojee Bwana,

uwe hodari na mwenye moyo mkuu,

nawe, umngojee Bwana.

Nami bado nina tumaini hili:

nitauona wema wa Bwana

katika nchi ya walio hai.

Mngojee Bwana,

uwe hodari na mwenye moyo mkuu,

nawe, umngojee Bwana.

Sala Ya Kusifu
Zaburi ya Daudi.

Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,

nimwogope nani?

Bwana ni ngome ya uzima wangu,

nimhofu nani?

Waovu watakaposogea dhidi yangu

ili wanile nyama yangu,

adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia,

watajikwaa na kuanguka.

Hata jeshi linizunguke pande zote,

moyo wangu hautaogopa;

hata vita vitokee dhidi yangu,

hata hapo nitakuwa na ujasiri.

Jambo moja ninamwomba Bwana,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Bwana

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Bwana

na kumtafuta hekaluni mwake.

Kwa kuwa siku ya shida,

atanihifadhi salama katika maskani yake,

atanificha uvulini mwa hema yake

na kuniweka juu kwenye mwamba.

Kisha kichwa changu kitainuliwa

juu ya adui zangu wanaonizunguka.

Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;

nitamwimbia Bwana na kumsifu.

Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana,

unihurumie na unijibu.

Moyo wangu unasema kuhusu wewe,

"Utafute uso wake!"

Uso wako, Bwana "Nitautafuta."

Usinifiche uso wako,

usimkatae mtumishi wako kwa hasira;

wewe umekuwa msaada wangu.

Usinikatae wala usiniache,

Ee Mungu Mwokozi wangu.

Hata kama baba yangu na mama wakiniacha,

Bwana atanipokea.

Nifundishe njia yako, Ee Bwana,

niongoze katika njia iliyonyooka

kwa sababu ya watesi wangu.

Usiniachilie kwa nia za adui zangu,

kwa maana mashahidi wa uongo

wameinuka dhidi yangu,

wakipumua ujeuri.

Nami bado nina tumaini hili:

nitauona wema wa Bwana

katika nchi ya walio hai.

Mngojee Bwana,

uwe hodari na mwenye moyo mkuu,

nawe, umngojee Bwana.

Espera paciente

Esperei com paciência no Senhor e Ele se inclinou para mim. Confie nele e descanse — Ele agirá no tempo certo.

Wimbo Wa Sifa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Nilimngoja Bwana kwa saburi,

naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,

kutoka matope na utelezi;

akaiweka miguu yangu juu ya mwamba

na kunipa mahali imara pa kusimama.

Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,

wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.

Wengi wataona na kuogopa

na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,

asiyewategemea wenye kiburi,

wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

Ee Bwana Mungu wangu,

umefanya mambo mengi ya ajabu.

Mambo uliyopanga kwa ajili yetu

hakuna awezaye kukuhesabia;

kama ningesema na kuyaelezea,

yangekuwa mengi mno kuyaelezea.

Dhabihu na sadaka hukuvitaka,

lakini umefungua masikio yangu;

sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukuzihitaji.

Ndipo niliposema, "Mimi hapa, nimekuja:

imeandikwa kunihusu katika kitabu.

Ee Mungu wangu,

natamani kuyafanya mapenzi yako;

sheria yako iko ndani ya moyo wangu."

Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,

sikufunga mdomo wangu,

Ee Bwana, kama ujuavyo.

Sikuficha haki yako moyoni mwangu;

ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.

Sikuficha upendo wako na kweli yako

mbele ya kusanyiko kubwa.

Ee Bwana, usizuilie huruma zako,

upendo wako na kweli yako daima vinilinde.

Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,

dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.

Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,

nao moyo unazimia ndani yangu.

Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;

Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,

waaibishwe na kufadhaishwa;

wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,

warudishwe nyuma kwa aibu.

Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini,

yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

Mioyo yetu humshangilia,

kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.

Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana,

tunapoliweka tumaini letu kwako.

Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,

katika neno lake naweka tumaini langu.

Nafsi yangu inamngojea Bwana

kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,

naam, kuliko walinzi

waingojeavyo asubuhi.

Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,

tumaini langu latoka kwake.

Mngojee Bwana,

na uishike njia yake.

Naye atakutukuza uirithi nchi,

waovu watakapokatiliwa mbali,

utaliona hilo.

Confiança e perseverança

Confie no Senhor de todo o coração. Sede pacientes na tribulação — o Senhor é fiel e cumprirá todas as suas promessas.

Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini,

mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha

Uvumilivu Katika Mateso

Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.

Kama mnavyojua, tunawahesabu kuwa wabarikiwa wale waliovumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu na mmeona kile ambacho hatimaye Bwana alimtendea. Bwana ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema.

Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni. Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. Maana,

"Wanadamu wote ni kama majani,

nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni;

majani hunyauka na maua huanguka,

lakini neno la Bwana ladumu milele."

Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba.

Mfano Wa Wanawali Kumi

"Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

"Usiku wa manane pakawa na kelele: Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!

"Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.

"Lakini wale wenye busara wakawajibu, Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.

"Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.

"Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!

"Lakini yeye bwana arusi akawajibu, Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!

"Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-