Publicidade

Estudar a Bíblia

Por Bíblia Online

Estudar a Bíblia é mergulhar na mente de Deus. A Palavra é lâmpada para os pés, espada do Espírito e alimento para a alma. O cristão que estuda cresce em sabedoria e maturidade.

A importância do estudo

Os bereanos eram mais nobres porque examinavam as Escrituras diariamente. Estudar a Bíblia é mandamento e privilégio.

Hawa Waberoya walikuwa waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.

Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli.

na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.

Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.

Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.

Meditar e guardar

Não se aparte a lei do Senhor da tua boca. Medita nela de dia e de noite para que cumpras tudo o que nela está escrito.

Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.

Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana

Neno lako ni taa ya miguu yangu

na mwanga katika njia yangu.

Kuipenda Sheria Ya Bwana

Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

Ninaitafakari mchana kutwa.

Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,

kwa kuwa nimezishika daima.

Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,

kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

Kutii Sheria Ya Bwana

Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?

Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,

usiniache niende mbali na amri zako.

Nimelificha neno lako moyoni mwangu

ili nisikutende dhambi.

Sifa ni zako, Ee Bwana,

nifundishe maagizo yako.

Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote

zinazotoka katika kinywa chako.

Ninafurahia kufuata sheria zako

kama mtu afurahiaye mali nyingi.

Ninatafakari maagizo yako

na kuziangalia njia zako.

Ninafurahia maagizo yako,

wala sitalipuuza neno lako.Bwana

Nitakusifu kwa moyo mnyofu

ninapojifunza sheria zako za haki.

Estudo diligente

Esdras preparou o coração para buscar e ensinar a lei. O estudo exige disciplina, constância e coração aberto.

Ezra alianza safari yake kutoka Babeli tangu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa maana mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake. Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya Bwana na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.

Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi. Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu Bwana Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

Utangulizi: Kusudi Na Kiini

Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:

Kwa kupata hekima na nidhamu;

kwa kufahamu maneno ya busara;

kwa kujipatia nidhamu na busara,

kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;

huwapa busara wajinga,

maarifa na akili kwa vijana;

wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,

wenye kupambanua na wapate mwongozo;

kwa kufahamu mithali na mifano,

misemo na vitendawili vya wenye hekima.

Faida Nyingine Za Hekima

Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,

bali zitunze amri zangu moyoni mwako,

kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako

na kukuletea mafanikio.

Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;

mshike, maana yeye ni uzima wako.

Kwa maana amri hizi ni taa,

mafundisho haya ni mwanga

na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

Proteção e crescimento

Quem ignora a Palavra perece. Toda Escritura é útil — crescei na graça e no conhecimento do nosso Senhor.

watu wangu wanaangamizwa

kwa kukosa maarifa,

"Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,

mimi nami nitakukataa wewe

usiwe kuhani kwangu mimi;

kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako

mimi nami sitawajali watoto wako.

Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.

Yesu akawajibu, "Je, hampotoki kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu?

Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

Basi, ninyi wapenzi, kwa kuwa mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na kuanguka kutoka kwenye uthabiti wenu. Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na milele! Amen.

Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa, wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-