Pular para o conteúdo
Publicidade

Família

Por Bíblia Online

A família é a primeira instituição criada por Deus. Ele a projetou para ser escola de amor, fé e formação de caráter. A Bíblia honra a família e nos ensina a cuidar dela.

Eu e minha casa

Eu e minha casa serviremos ao Senhor. A família que serve a Deus juntos permanece unida e fortalecida em todas as circunstâncias.

Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana."

Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana."

Wakamjibu, "Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako."

Bwana Mungu wetu na awe pamoja nasi kama alivyokuwa na baba zetu, kamwe asituache wala kutukataa.

Criar os filhos

Instrui a criança no caminho em que deve andar. O lar é a primeira escola de fé e obediência.

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,

naye hataiacha hata akiwa mzee.

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,

naye hataiacha hata akiwa mzee.

Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu

Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,

wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,

na mkufu wa kuipamba shingo yako.

Onyo Dhidi Ya Uasherati

Mwanangu, zishike amri za baba yako,

wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi,

Honrar e amar

Honra teu pai e tua mãe. A família funciona com perdão, paciência e amor incondicional entre todos os seus membros.

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako."

Yesu Afundisha Kuhusu Talaka

Yesu alipomaliza kusema maneno haya, aliondoka Galilaya, akaenda sehemu za Uyahudi, ngʼambo ya Mto Yordani. Umati mkubwa wa watu ukamfuata, naye akawaponya huko.

Baadhi ya Mafarisayo wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, "Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?"

Akawajibu, "Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, naye akasema, Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."

Wakamuuliza, "Kwa nini basi Mose aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?"

Yesu akawajibu, "Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini."

Wanafunzi wake wakamwambia, "Kama hali ndiyo hii kati ya mume na mke, ni afadhali mtu asioe!"

Yesu akawaambia, "Si watu wote wanaoweza kupokea neno hili, isipokuwa wale tu waliojaliwa na Mungu. Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo; wengine wamefanywa matowashi na wanadamu; na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee."

Yesu Awabariki Watoto Wadogo

Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Yesu ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta.

Yesu akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa." Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko.

Kijana Tajiri

Mtu mmoja akamjia Yesu na kumuuliza, "Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?"

Yesu akamjibu, "Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri."

Yule mtu akamuuliza, "Amri zipi?"

Yesu akamjibu, "Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako."

Yule kijana akasema, "Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?"

Yesu akamwambia, "Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate."

Yule kijana aliposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Hatari Za Utajiri

Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Amin, nawaambia, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Tena nawaambia, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu."

Wanafunzi wake waliposikia haya, walishangaa sana na kuuliza, "Ni nani basi awezaye kuokoka?"

Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu."

Ndipo Petro akamjibu, "Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata! Tutapata nini basi?"

Yesu akawaambia, "Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.

Ikiwa mtu atasema, "Nampenda Mungu," lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona?

Cuidar da família

Quem não cuida dos seus negou a fé. A família é responsabilidade sagrada — prover, proteger e abençoar é mandamento divino.

Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.

Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.

Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu.

Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa

Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi.

Wana ni urithi utokao kwa Bwana,

watoto ni zawadi kutoka kwake.

Kama mishale mikononi mwa shujaa

ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

Heri mtu ambaye podo lake

limejazwa nao.

Hawataaibishwa wanaposhindana

na adui zao langoni.

Lakini kutoka milele hata milele

upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,

nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

kwa wale walishikao agano lake

na kukumbuka kuyatii mausia yake.

Lakini kutoka milele hata milele

upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,

nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

kwa wale walishikao agano lake

na kukumbuka kuyatii mausia yake.

Sifa Za Pendo La Undugu

Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza

wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

Unidade familiar

A coroa dos velhos são os filhos dos filhos. O casamento, os filhos e a comunhão familiar são bênçãos de Deus.

Wana wa wana ni taji la wazee,

nao wazazi ni fahari ya watoto wao.

Wana wa wana ni taji la wazee,

nao wazazi ni fahari ya watoto wao.

Rafiki hupenda wakati wote

naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,

bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.

Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,

tena usiende nyumbani mwa ndugu yako

wakati umepatwa na maafa.

Bora jirani wa karibu

kuliko ndugu aliye mbali.

Mwanangu, kama moyo wako una hekima,

basi moyo wangu utafurahi,

Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,

naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

Mithali Za Solomoni

Mithali za Solomoni:

Mwana mwenye hekima

huleta furaha kwa baba yake,

lakini mwana mpumbavu

huleta huzuni kwa mama yake.

Maliza kazi zako za nje,

nawe uweke mashamba yako tayari,

baada ya hayo, jenga nyumba yako.

Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu,

bali yeye achukiaye rushwa ataishi.

Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo,

naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.

Casamento e família

O homem deixará pai e mãe e se unirá à sua mulher. A família começa no casamento — aliança sagrada diante de Deus.

Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Mungu akawabariki na akawaambia, "Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi."

Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua.

Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."

Basi ikiwa ninyi mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wale wamwombao!"

"Je, mama aweza kumsahau mtoto

aliyeko matitini mwake akinyonya,

wala asiwe na huruma

juu ya mtoto aliyemzaa?

Ingawa anaweza kusahau,

mimi sitakusahau wewe!

Tazama, nimekuchora kama muhuri

katika vitanga vya mikono yangu,

kuta zako zi mbele yangu daima.

Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.

Seja o primeiro