Homem de Deus
O homem de Deus é aquele que busca a justiça, a piedade, a fé e o amor. A Bíblia apresenta modelos de homens íntegros que andaram com Deus e marcaram a história.
Características do homem de Deus
O homem de Deus foge das paixões e segue a justiça, a piedade, a fé, o amor, a perseverança e a mansidão.
Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.
Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.
Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, kuweni mashujaa kuweni hodari. Fanyeni kila kitu katika upendo.
Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu.
Bwana anataka nini kwako?
Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,
na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.
Exemplos bíblicos
Noé era justo e íntegro entre seus contemporâneos. Jó era homem reto que temia a Deus e se desviava do mal.
Hivi ndivyo vizazi vya Noa.
Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.
Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia kwake watu wote waweze kuamini.
Mtu wa ufahamu huitazama hekima,
lakini macho ya mpumbavu huhangaika
hadi kwenye miisho ya dunia.
Viver como filho de Deus
Quem faz a vontade de Deus é eleito. Medite na Palavra e ande nos caminhos do Senhor como verdadeiro discípulo.
Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.
Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
Sifa ni zako, Ee Bwana,
nifundishe maagizo yako.
Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote
zinazotoka katika kinywa chako.
Ninafurahia kufuata sheria zako
kama mtu afurahiaye mali nyingi.
Ninatafakari maagizo yako
na kuziangalia njia zako.
Ninafurahia maagizo yako,
wala sitalipuuza neno lako.Bwana
Heri mtu yule ambaye
haendi katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
Bali huifurahia sheria ya Bwana,
naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.
Mtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lolote afanyalo hufanikiwa.
Sivyo walivyo waovu!
Wao ni kama makapi
yapeperushwayo na upepo.
Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki,
bali njia ya waovu itaangamia.
Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, ili mfanywe upya roho na nia zenu, mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.