Publicidade

Homem

Por Bíblia Online

A Bíblia fala sobre o homem como criação de Deus — feito à sua imagem e semelhança, mas também frágil, mortal e necessitado de redenção.

Criado à imagem de Deus

Deus criou o homem à sua imagem. Mas pelo pecado, o homem caiu e passou a depender da graça para ser restaurado.

Ndipo Mungu akasema, "Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi."

Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,

kwa mfano wa Mungu alimuumba;

mwanaume na mwanamke aliwaumba.

Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani.

Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na kupitia dhambi hii mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi:

Kwa hiyo imeandikwa, "Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai"; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima. Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho. Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. Kama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. Kama vile tulivyochukua mfano wa mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua mfano wa yule mtu aliyetoka mbinguni.

Fragilidade humana

O homem nascido de mulher é de poucos dias e cheio de inquietação. Deus conhece nossa fragilidade e cuida de nós.

"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke

siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.

‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu?

Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?

"Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki,

kwamba unamtia sana maanani,

Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema:

"Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,

binadamu ni nani hata unamjali?

Hatua za mtu huongozwa na Bwana.

Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?

Renovação e chamado

Despojados do velho homem e revestidos do novo, somos chamados a buscar a justiça, a piedade e o amor.

Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, ili mfanywe upya roho na nia zenu, mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

kwa kuibatilisha ile sheria pamoja na amri zake na maagizo yake alipoutoa mwili wake, ili apate kufanya ndani yake mtu mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo akifanya amani,

Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.

Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, niliwaza kama mtoto, nilifikiri kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto.

Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana,

naye huyapima mapito yake yote.

Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,

bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

A confiança errada

Maldito o homem que confia no homem. O homem de duplo ânimo é instável em todos os seus caminhos.

Hili ndilo asemalo Bwana:

"Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu,

ategemeaye mwenye mwili

kwa ajili ya nguvu zake,

ambaye moyo wake

umemwacha Bwana.

Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana. Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.

Usimkemee mzee kwa ukali bali umshawishi kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako;

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-