Honrar os pais
Honrar pai e mãe é mandamento de Deus com promessa de vida longa e feliz. A Bíblia ensina que respeitar, obedecer e cuidar dos pais é dever sagrado dos filhos.
O mandamento com promessa
Honra a teu pai e a tua mãe para que vá bem contigo e vivas muito tempo sobre a terra. É o primeiro mandamento com promessa.
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.
Watoto na wazazi
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
Obedecer e respeitar
Filhos, obedecei a vossos pais no Senhor. Ouvir a instrução do pai e não desprezar o ensino da mãe traz sabedoria.
Maonyo juu ya kushirikiana na waovu
Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako,
Maonyo juu ya kushirikiana na waovu
Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako,
Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,
Na mikufu shingoni mwako.
Ushauri wa mzazi
Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu,
Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;
Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.
Msikilize baba yako aliyekuzaa,
Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huivunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huivunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, chochote kikupasacho nikusaidie kwacho nakitoa wakfu, basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
Consequências da desonra
A Bíblia adverte severamente contra a desonra aos pais. Quem amaldiçoa ou agride os pais enfrenta consequências sérias.
Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye,
Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.
Amlaaniye babaye au mamaye,
Taa yake itazimika katika giza kuu.
Jicho la mtu amdhihakiye babaye,
Na kudharau kumtii mamaye;
Kunguru wa bondeni wataling’oa,
Na vifaranga vya tai watalila.
Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
Uovu katika siku za mwisho
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
Cuidar dos pais
Quem não cuida dos seus, principalmente de sua família, negou a fé. Honrar os pais inclui respeitar os idosos.
Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.