Publicidade

Jovens

Por Bíblia Online

Deus tem planos maravilhosos para os jovens. A Bíblia os convida a consagrar a juventude ao Senhor, crescer em sabedoria e ser exemplo para todos em fé, palavra, conduta e amor.

Ninguém despreze a tua mocidade

Paulo exortou Timóteo: sê exemplo dos fiéis na palavra, no procedimento, no amor, no espírito, na fé e na pureza.

Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.

Vivyo hivyo, himiza vijana wawe na kiasi.

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, "upate baraka na uishi siku nyingi duniani."

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi,

Lembrar do Criador na juventude

Lembra-te do teu Criador nos dias da tua mocidade. A sabedoria ganha cedo produz frutos duradouros na vida inteira.

Mkumbuke Muumba wako

siku za ujana wako,

kabla hazijaja siku za taabu,

wala haijakaribia miaka utakaposema,

"Mimi sifurahii hiyo":

Mkumbuke Muumba wako

siku za ujana wako,

kabla hazijaja siku za taabu,

wala haijakaribia miaka utakaposema,

"Mimi sifurahii hiyo":

kabla jua na nuru,

nao mwezi na nyota havijatiwa giza,

kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;

siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka,

nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha,

wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache,

nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana,

moyo wako na ukupe furaha

katika siku za ujana wako.

Fuata njia za moyo wako

na chochote macho yako yaonayo,

lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote

Mungu atakuleta hukumuni.

Kwa hiyo basi, ondoa wasiwasi moyoni mwako

na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako,

kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.

Força e promessa

Os jovens renovam suas forças quando esperam no Senhor. Deus levanta jovens com visões e sonhos para transformar o mundo.

Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

bali wale wamtumainio Bwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

"Hata itakuwa, baada ya hayo,

nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

wazee wenu wataota ndoto,

na vijana wenu wataona maono.

Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu.

Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.

Mwisho wa muda uliowekwa na mfalme kuwaingiza kwake, mkuu wa maafisa akawaleta mbele ya Mfalme Nebukadneza. Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme.

Utukufu wa vijana ni nguvu zao,

mvi ni fahari ya uzee.

Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,

kama tabia yake ni safi na adili.

Guardar o caminho

Como purificará o jovem seu caminho? Guardando-o segundo a tua Palavra. A Escritura na juventude guarda do pecado a vida inteira.

Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?

Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

Nimelificha neno lako moyoni mwangu

ili nisikutende dhambi.

Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi,

tegemeo langu tangu ujana wangu.

wanaume vijana na wanawali,

wazee na watoto.

Wote na walisifu jina la Bwana,

kwa maana jina lake pekee limetukuka,

utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.

Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:

Kwa kupata hekima na nidhamu;

kwa kufahamu maneno ya busara;

kwa kujipatia nidhamu na busara,

kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;

huwapa busara wajinga,

maarifa na akili kwa vijana;

Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima,

weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.

Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo,

au wale walao nyama kwa pupa,

kwa maana walevi na walafi huwa maskini,

nako kusinzia huwavika matambara.

Msikilize baba yako, aliyekuzaa,

wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.

Coragem e vocação

Deus chamou jovens como Jeremias e Josué para grandes missões. A juventude não é desculpa — é oportunidade de servir poderosamente.

Nami nikasema, "Aa, Bwana Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu."

Lakini Bwana akaniambia, "Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe," asema Bwana.

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Bwana, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nitaonekana kwenu," asema Bwana, "nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni," asema Bwana.

Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Mose mtumishi wangu, usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote uendako. Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi. Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako."

Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa,

"Mungu huwapinga wenye kiburi,

lakini huwapa wanyenyekevu neema."

Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.

Nawaandikia ninyi akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana,

kwa sababu mna nguvu,

na neno la Mungu linakaa ndani yenu,

nanyi mmemshinda yule mwovu.

Basi na tuenende kwa adabu kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa kufanya karamu za ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.

Ni vyema mtu kuchukua nira

bado angali kijana.

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-