Ler a Bíblia
Ler a Bíblia é essencial para a vida cristã. A Escritura é lâmpada para os pés, alimento para a alma e espada do Espírito. O cristão que lê a Bíblia é transformado pela Palavra.
A importância de ler
Meditar na Palavra dia e noite traz prosperidade e bom sucesso. Ler a Bíblia ilumina o entendimento e fortalece a fé.
Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Neno lako ni taa ya miguu yangu
na mwanga katika njia yangu.
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,
kunampa mjinga ufahamu.
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.
Ninaitafakari mchana kutwa.
Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,
kwa kuwa nimezishika daima.
Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,
kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.
Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
A Escritura é inspirada
Toda a Escritura é útil para ensinar, corrigir e instruir em justiça. Examine as Escrituras — nelas encontramos a vida eterna.
Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.
Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.
Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.
Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.
Estudar com diligência
Os bereanos eram mais nobres porque examinavam as Escrituras diariamente. O estudo dedicado da Bíblia produz maturidade espiritual.
Hawa Waberoya walikuwa waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.
Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya Bwana na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.
Walisoma kutoka kile Kitabu cha Sheria ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa.
Yesu akawajibu, "Je, hampotoki kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu?
Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.
Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu
na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,
kutega sikio lako kwenye hekima
na kuweka moyo wako katika ufahamu,
na kama ukiita busara
na kuita kwa sauti ufahamu,
na kama utaitafuta kama fedha
na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
ndipo utakapoelewa kumcha Bwana
na kupata maarifa ya Mungu.
Kwa maana Bwana hutoa hekima,
na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.