A mulher virtuosa
A mulher virtuosa de Provérbios 31 é um retrato de excelência. Seu valor excede o de rubis — ela é sábia, trabalhadora, generosa e teme ao Senhor acima de tudo.
Uma joia rara
Mulher virtuosa, quem a achará? Seu valor excede o de rubis. Ela é o coração da família e a força do lar.
Wimbo kwa mke Mwema
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
Wimbo kwa mke Mwema
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
Tena huamka, kabla usiku haujaisha;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
Mwanamke mwema ni taji la mumewe;
Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Caráter acima da aparência
Enganosa é a graça e vã é a formosura, mas a mulher que teme ao Senhor será louvada. A verdadeira beleza é interior.
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.