Mulher
A Bíblia celebra a mulher como obra-prima da criação divina. Ela é elogiada por sua sabedoria, força, beleza interior e papel fundamental na família e na sociedade.
A mulher na criação
Deus criou o homem e a mulher à sua imagem. A mulher foi formada como ajudadora idônea — parceira de igual dignidade e valor.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
Virtude e caráter
A beleza é vã e a formosura passageira, mas a mulher que teme ao Senhor é digna de louvor. Seu caráter é seu maior tesouro.
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Mwanamke mwema ni taji la mumewe;
Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.
Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima;
Na watu wakali hushika mali siku zote.
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;
Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Sabedoria e serviço
As mulheres da Bíblia foram líderes, profetisas e discípulas fiéis. Jesus honrou as mulheres e as incluiu em seu ministério.
Baadhi ya wanawake waandamana na Yesu
Ikawa baada ya hayo alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza Habari Njema ya ufalme wa Mungu; na wale Kumi na Wawili walikuwa pamoja naye, na wanawake kadhaa ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
Wake na waume
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.
Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; wasiwe wachongezi; ila wawe watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.