Namoro e sexo
Namoro e sexo são temas que a Bíblia trata com clareza e sem tabus. Deus criou o sexo como bênção dentro do casamento e nos chama à pureza fora dele.
Pureza sexual
A vontade de Deus é a santificação. Cada um saiba controlar seu próprio corpo em santidade e honra, não na paixão do desejo.
Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.
"Chakula ni cha tumbo, na tumbo ni la chakula": lakini Mungu ataviangamiza vyote viwili. Mwili haukuumbwa kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya Bwana na Bwana kwa ajili ya mwili.
Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.
Arrependimento e restauração
Bem-aventurado aquele cujo pecado é perdoado. Deus restaura os que se arrependem e cria neles um coração limpo e renovado.
Furaha Ya Msamaha
Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,
ambaye dhambi zake zimefunikwa.
Heri mtu yule ambaye Bwana
hamhesabii dhambi,
na ambaye rohoni mwake
hamna udanganyifu.
Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa
kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.
Usiku na mchana
mkono wako ulinilemea,
nguvu zangu zilinyonywa
kama vile katika joto la kiangazi.
Kisha nilikujulisha dhambi yangu
wala sikuficha uovu wangu.
Nilisema, "Nitaungama
makosa yangu kwa Bwana."
Ndipo uliponisamehe
hatia ya dhambi yangu.
Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe
wakati unapopatikana,
hakika maji makuu yatakapofurika
hayatamfikia yeye.
Unioshe na uovu wangu wote
na unitakase dhambi yangu.
Kwa maana ninajua makosa yangu,
na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi
na kufanya yaliyo mabaya machoni pako,
ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo,
na kuwa na haki utoapo hukumu.
Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi,
unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
Unipe kusikia furaha na shangwe,
mifupa uliyoiponda na ifurahi.
Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu,
na uufute uovu wangu wote.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
Usinitupe kutoka mbele zako
wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
Unirudishie tena furaha ya wokovu wako,
unipe roho ya utii, ili initegemeze.