Publicidade

Não temas

Por Bíblia Online

'Não temas' é uma das frases mais repetidas na Bíblia. Deus a pronuncia nos momentos de maior temor, lembrando que sua presença e poder são maiores que qualquer ameaça.

Deus está contigo

Não temas, porque eu sou contigo. Deus repete essa promessa em cada crise, guerra e desafio que seus filhos enfrentam.

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

nikushikaye mkono wako wa kuume

na kukuambia, Usiwe na hofu,

nitakusaidia.

Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu,

ee Israeli uliye mdogo,

kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia," asema Bwana,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Wewe uletaye habari njema Sayuni,

panda juu ya mlima mrefu.

Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,

inua sauti yako kwa kupiga kelele,

inua sauti, usiogope;

iambie miji ya Yuda,

"Yuko hapa Mungu wenu!"

Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako."

Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."

Baada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono:

"Usiogope, Abramu.

Mimi ni ngao yako,

na thawabu yako kubwa sana."

Coragem diante do perigo

Não tenhas medo — o Senhor teu Deus está no meio de ti, poderoso para salvar. Ele luta por nós e dá forças aos medrosos.

Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu,

"Usiogope, ee Sayuni;

usiiache mikono yako ilegee.

Bwana Mungu wako yu pamoja nawe,

yeye ni mwenye nguvu kuokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Nabii akajibu, "Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi zaidi kuliko wale walio pamoja nao."

Kisha Elisha akaomba, "Ee Bwana, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona." Ndipo Bwana akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto, yamemzunguka Elisha pande zote.

Usiogope, ee nchi;

furahi na kushangilia.

Hakika Bwana ametenda mambo makubwa.

Lakini Bwana akaniambia, "Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe," asema Bwana.

Usiku mmoja Bwana akamwambia Paulo katika maono, "Usiogope, lakini endelea kusema wala usinyamaze, kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia ili kukudhuru, kwa kuwa ninao watu wengi katika mji huu ambao ni watu wangu."

Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao, usiogope, ingawa michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ingawa wao ni nyumba ya uasi. Wewe lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikiliza au hawasikilizi, kwa kuwa wao ni watu waasi.

Fé que vence o medo

O medo não vem de Deus. Jesus disse: não temas, crê somente! A fé dissipa o medo e nos conecta ao poder de Deus.

Aliposikia hayo waliyosema, Yesu akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, "Usiogope. Amini tu."

Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.

Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, "Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Ndipo malaika akamwambia, "Usiogope, Maria, umepata kibali kwa Mungu.

Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni mwa Yesu na kumwambia, "Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!"

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-