Pular para o conteúdo
Publicidade

Obediência aos pais

Por Bíblia Online

A obediência aos pais é mandamento divino com promessa de vida longa. A Bíblia valoriza a honra filial e ensina os filhos a respeitar e obedecer aos pais com amor.

Honrar pai e mãe

O quinto mandamento ordena honrar pai e mãe. É o primeiro mandamento com promessa: para que vá bem e vivas muito na terra.

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

Waheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi Bwana Mungu wako anayokupa.

Kwa maana Mungu alisema, Waheshimu baba yako na mama yako,na, Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.

Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, "upate baraka na uishi siku nyingi duniani."

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

Obedecer e respeitar

Filhos, obedecei a vossos pais no Senhor. A obediência filial é expressão de amor e temor a Deus.

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.

Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu

Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,

wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,

na mkufu wa kuipamba shingo yako.

Onyo Dhidi Ya Uasherati

Mwanangu, zishike amri za baba yako,

wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

Yafunge katika moyo wako daima,

yakaze kuizunguka shingo yako.

Wakati utembeapo, yatakuongoza;

wakati ulalapo, yatakulinda;

wakati uamkapo, yatazungumza nawe.

Kwa maana amri hizi ni taa,

mafundisho haya ni mwanga

na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote

Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu;

sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu.

Ninawapa mafundisho ya maana,

kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu.

Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu,

ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu,

baba alinifundisha akisema,

"Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;

yashike maagizo yangu na wewe utaishi.

Pata hekima, pata ufahamu;

usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.

Usimwache hekima naye atakuweka salama;

mpende, naye atakulinda.

Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu

Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,

bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,

naye hataiacha hata akiwa mzee.

Disciplina e consequências

A vara e a repreensão dão sabedoria. A Bíblia adverte sobre as consequências sérias da rebeldia e desonra aos pais.

Fimbo ya maonyo hutia hekima,

bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo

humwaibisha mama yake.

Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake

ni mwana aletaye aibu na fedheha.

"Jicho lile limdhihakilo baba,

lile linalodharau kumtii mama,

litangʼolewa na kunguru wa bondeni,

litaliwa na tai.

"Yeyote amshambuliaye baba yake au mama yake ni lazima auawe.

Mwana Mwasi

Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi, baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake. Watawaambia wazee, "Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi." Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,

taa yake itazimwa katika giza nene.

Vumilieni taabu kwa ajili ya kufunzwa adabu. Mungu anawatendea ninyi kama watoto wake, kwa maana ni mtoto yupi asiyeadibishwa na mzazi wake?

Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo impendezavyo Mungu.

Seja o primeiro