Publicidade

Orgulho

Por Bíblia Online

O orgulho é um dos pecados mais condenados na Bíblia. Deus resiste aos soberbos, mas dá graça aos humildes. A humildade é o caminho da honra verdadeira.

Deus resiste ao soberbo

A soberba precede a ruína e o orgulho antecede a queda. Deus abomina o coração altivo e promete humilhar quem se exalta.

Kiburi hutangulia maangamizi,

roho ya majivuno hutangulia maanguko.

Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo.

Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.

Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,

bali mwisho wake huelekeza mautini.

Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;

ninachukia kiburi na majivuno,

tabia mbaya na mazungumzo potovu.

Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,

bali unyenyekevu huja na hekima.

Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,

bali unyenyekevu huja na hekima.

Kiburi cha mtu humshusha,

bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu

hupata heshima.

Kiburi cha mtu humshusha,

bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu

hupata heshima.

Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,

bali unyenyekevu hutangulia heshima.

Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,

bali unyenyekevu hutangulia heshima.

Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi,

bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

Humildade como caminho

Humilhai-vos diante do Senhor e Ele vos exaltará. A grandeza no Reino vem pelo serviço humilde, não pela autopromoção.

Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema:

"Mungu huwapinga wenye kiburi,

lakini huwapa wanyenyekevu neema."

Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.

Umaskini Na Utajiri

Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa. Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani.

Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa,

"Mungu huwapinga wenye kiburi,

lakini huwapa wanyenyekevu neema."

Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.

Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa."

Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake. Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.

Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu:

Os perigos do orgulho

O orgulho cega, gera contendas e afasta de Deus. A Escritura adverte contra a soberba da vida e a vã glória mundana.

Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu.

Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.

Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.

Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, ili mtu yeyote asijisifu mbele zake.

Lakini, "Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana." Kwa maana si yeye ajisifuye mwenyewe akubaliwaye, bali yeye ambaye Bwana humsifu.

Akaendelea kusema, "Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi."

Kiburi huzalisha magomvi tu,

bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

Unyenyekevu na kumcha Bwana

huleta utajiri, heshima na uzima.

Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.

O olhar de Deus

O Senhor não olha como o homem. Ele vê o coração e se agrada dos quebrantados de espírito e dos que tremem diante da sua Palavra.

Lakini Bwana akamwambia Samweli, "Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. Bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana hutazama moyoni."

"Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo

wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi,

kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye,

na kwa yeye matendo hupimwa.

Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?"

asema Bwana.

"Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.

Mfalme wa Israeli akajibu, "Mwambieni, Yule anayevaa mavazi ya vita asije akajisifu kama yule anayevua.’ "

Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu.

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-