Publicidade

Palavras de conforto

Por Bíblia Online

Deus é o Deus de todo conforto. Ele consola os que choram, restaura os quebrantados e promete que a dor presente dará lugar à alegria eterna.

O Deus de toda consolação

Bendito seja o Deus e Pai de nosso Senhor Jesus Cristo, Pai das misericórdias e Deus de toda consolação, que nos consola em todas as tribulações.

Mungu Wa Faraja Yote

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.

Mungu Wa Faraja Yote

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo. Kama tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata. Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki katika faraja yetu.

Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo.

Kwa maana hakupuuza wala kudharau

mateso ya aliyeonewa;

hakumficha uso wake

bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.

Bwana yu karibu na waliovunjika moyo,

na huwaokoa waliopondeka roho.

Promessas de restauração

Deus sarará o quebrantado de coração e atará as suas feridas. Quem semeia em lágrimas, colherá com júbilo.

Anawaponya waliovunjika mioyo

na kuvifunga vidonda vyao.

Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

bali upendo wake hudumu siku zote.

Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

lakini asubuhi kukawa na furaha.

Mungu Yuko Pamoja Nasi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi.

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Mtwike Bwana fadhaa zako,

naye atakutegemeza,

hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

Andika maombolezo yangu,

orodhesha machozi yangu katika gombo lako:

je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?

Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa,

ni ngome imara wakati wa shida.

Bwana ni mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

Mungu wangu ni mwamba,

ambaye kwake ninakimbilia.

Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,

ngome yangu.

Paz e descanso

Jesus disse: 'Vinde a mim, todos os cansados e sobrecarregados, e eu vos aliviarei.' A paz de Deus que excede todo entendimento guarda o coração.

Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo

"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo

"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Heri wale wanaohuzunika,

maana hao watafarijiwa.

Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."

Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Esperança eterna

Deus enxugará toda lágrima. A dor presente é momentânea, mas a glória futura é eterna. O Senhor transforma luto em dança.

Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, "Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita."

Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, "Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!" Kisha akasema, "Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli."

Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Mwaka Wa Upendeleo Wa Bwana

Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,

kwa sababu Bwana amenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,

na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

kuwafariji wote waombolezao,

na kuwapa mahitaji

wale wanaohuzunika katika Sayuni,

ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

Nao wataitwa mialoni ya haki,

pando la Bwana,

ili kuonyesha utukufu wake.

Kama mama anavyomfariji mtoto wake,

ndivyo nitakavyokufariji wewe,

nawe utafarijiwa huko Yerusalemu."

Nunca sozinhos

Deus nunca nos abandona. Ele está ao nosso lado em cada vale, segura nossa mão e promete que o choro não durará para sempre.

Bwana mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."

Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,

"Kamwe sitakuacha,

wala sitakupungukia."

Bwana ni Mwema,

kimbilio wakati wa taabu.

Huwatunza wale wanaomtegemea,

Bwana Mungu wako yu pamoja nawe,

yeye ni mwenye nguvu kuokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Bwana, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.

Kwa hiyo, wale wanaoteswa kulingana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu, huku wakizidi kutenda mema.

Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.

Hata kama nikipita katikati

ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya,

kwa maana wewe upo pamoja nami;

fimbo yako na mkongojo wako

vyanifariji.

Jambo moja ninamwomba Bwana,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Bwana

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Bwana

na kumtafuta hekaluni mwake.

Kwa kuwa siku ya shida,

atanihifadhi salama katika maskani yake,

atanificha uvulini mwa hema yake

na kuniweka juu kwenye mwamba.

Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:

Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

Huwainua juu wanyonge,

nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama.

Yesu akasema, "Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao.

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-