Pão
O pão é símbolo central na Bíblia: do maná no deserto ao pão da vida — Jesus. A Escritura usa o pão para ensinar sobre provisão divina, comunhão e dependência espiritual.
O maná do céu
Deus alimentou Israel no deserto com pão do céu. O maná era diário, fiel e suficiente — retrato da provisão constante de Deus.
Bwana akamwambia Mose, "Nimesikia manungʼuniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua ya kwamba Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ "
Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na tabaka la umande kuzunguka kambi. Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. Waisraeli walipoona, wakaambiana, "Hiki ni nini?" Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Mose akawaambia, "Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle.
Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali.
Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu
na kufungua milango ya mbingu,
akawanyeshea mana ili watu wale;
aliwapa nafaka ya mbinguni.
Watu walikula mkate wa malaika,
akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula.
Huyafanya majani ya mifugo yaote,
na mimea kwa watu kulima,
wajipatie chakula kutoka ardhini:
divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu,
mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake,
na mkate wa kutia mwili nguvu.
O pão da vida
Jesus declarou: 'Eu sou o pão da vida.' Quem vem a Ele nunca terá fome, e quem nele crê jamais terá sede. Ele é o sustento eterno.
Yesu akawaambia, "Amin, amin nawaambia, si Mose aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima."
Wakamwambia, "Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote."
Yesu akawaambia, "Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe.
Mimi ni mkate wa uzima. Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu yeyote akiula, hatakufa. Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu."
Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana.
Lakini Yesu akajibu, "Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ "
Partilha e comunhão
O partir do pão une o corpo de Cristo. Na Ceia, na generosidade e na partilha, expressamos a comunhão com Deus e uns com os outros.
Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, "Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu."
Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo.
Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja.
"Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba:
" ‘Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike
hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupatie riziki yetu
ya kila siku.
Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa
kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.
Lakini Yesu akawajibu, "Ninyi wapeni chakula."
Wakamwambia, "Je, twende tukanunue mikate ya dinari 200 ili tuwape watu hawa wale?"
Akawauliza, "Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie."
Walipokwisha kujua wakarudi, wakamwambia, "Kuna mikate mitano na samaki wawili."
Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani, nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na wengine hamsini hamsini. Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. Watu wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Provisão divina
O justo não é desamparado e seus descendentes não mendigam pão. Deus provê com fidelidade o alimento de cada dia.
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,
lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa
au watoto wao wakiombaomba chakula.
Chachu Ya Mafarisayo Na Masadukayo
Wanafunzi wake walipofika ngʼambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. Yesu akawaambia, "Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo."
Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, "Ni kwa sababu hatukuleta mikate."
Yesu, akifahamu majadiliano yao, akauliza, "Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? Au ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo." Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
Mkate Juu Ya Maji
Tupa mkate wako juu ya maji,
kwa maana baada ya siku nyingi
utaupata tena.
Wape sehemu watu saba, naam hata wanane,
kwa maana hujui ni baa gani
litakalokuwa juu ya nchi.