Publicidade

Gravidez e maternidade

Por Bíblia Online

Gravidez e maternidade são bênçãos celebradas na Bíblia. Deus forma cada criança no ventre, cuida da mãe e da família, e abençoa a geração dos justos.

Filhos são herança do Senhor

Deus abençoa a fertilidade e o crescimento das famílias. Cada criança é obra de suas mãos, conhecida e amada antes mesmo de nascer.

Mtabarikiwa kuliko mataifa mengine yote, hakuna wanaume wala wanawake kwenu watakaokosa watoto, wala mifugo yenu haitakuwa tasa.

lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi.

Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,

kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

Umbile langu halikufichika kwako,

nilipoumbwa mahali pa siri.

Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

Siku zangu zote ulizonipangia

ziliandikwa katika kitabu chako

kabla haijakuwepo hata moja.

Wana ni urithi utokao kwa Bwana,

watoto ni zawadi kutoka kwake.

Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa

na nisizalishe?" asema Bwana.

"Je, nifunge tumbo la uzazi

wakati mimi ndiye nizalishaye?"

asema Mungu wako.

Força e cuidado na gravidez

Deus dá forças à mulher grávida e a sustenta em cada etapa. Sua graça é suficiente e seu poder se aperfeiçoa na fraqueza.

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Lakini aliniambia, "Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu." Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

Nitegee sikio lako,

uje uniokoe haraka;

uwe kwangu mwamba wa kimbilio,

ngome imara ya kuniokoa.

Kutoka miisho ya dunia ninakuita,

ninaita huku moyo wangu unadhoofika;

uniongoze kwenye mwamba

ule ulio juu kuliko mimi.

Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:

Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake

na kuwachukua karibu na moyo wake,

huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.

"Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo,

ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli,

ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba,

nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.

Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

Nimewahuluku, nami nitawabeba,

nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.

A bênção da maternidade

A Bíblia honra a maternidade como ministério sagrado. As mães são instrumentos de Deus para formar vidas e transmitir a fé.

Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.

Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa,

mumewe pia humsifu, akisema:

Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, "Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume."

Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi.

Isaki akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Bwana akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba.

Hivyo wakati ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa mwana. Hana akamwita jina lake Samweli, akasema, "Kwa kuwa nilimwomba kwa Bwana."

Proteção divina

Deus protege a mãe e o bebê, guardando-os de todo mal. Ele acompanha cada momento com ternura e fidelidade.

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

Nitasema kumhusu Bwana, "Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ambaye ninamtumaini."

Bwana atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

"Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

nilikuweka uwe nabii kwa mataifa."

"Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai,

"Je, mama aweza kumsahau mtoto

aliyeko matitini mwake akinyonya,

wala asiwe na huruma

juu ya mtoto aliyemzaa?

Ingawa anaweza kusahau,

mimi sitakusahau wewe!

Esperança e promessa

A maternidade é caminho de esperança. Como Sara, Ana e Isabel, as mães encontram na fé a força para aguardar as promessas de Deus.

Kwa imani Abrahamu, ingawa alikuwa mzee wa umri, naye Sara mwenyewe aliyekuwa tasa, alipokea uwezo wa kuwa baba kwa sababu alimhesabu Mungu aliyemwahidi kuwa mwaminifu na kwamba angetimiza ahadi yake.

Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa."

Naye Maria akasema:

"Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

nayo roho yangu inamfurahia

Mungu Mwokozi wangu,

kwa kuwa ameangalia kwa fadhili

unyonge wa mtumishi wake.

Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa,

kwa maana yeye Mwenye Nguvu

amenitendea mambo ya ajabu:

jina lake ni takatifu.

Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,

akiwa mama watoto mwenye furaha.

Msifuni Bwana.

Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake."

Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao

ndani ya nyumba yako;

wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni

kuizunguka meza yako.

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-