Preservação das escrituras
A Palavra de Deus permanece para sempre. As Escrituras foram preservadas por Deus ao longo dos milênios para instrução, consolação e guia de todas as gerações.
A Palavra eterna
Céus e terra passarão, mas as palavras de Deus jamais passarão. Sua Palavra é eterna, infalível e imutável — a verdade que sustenta tudo.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwenye Sheria, mpaka kila kitu kiwe kimetimia.
Majani hunyauka na maua huanguka,
lakini neno la Mungu wetu ladumu milele."
Maana,
"Wanadamu wote ni kama majani,
nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni;
majani hunyauka na maua huanguka,
lakini neno la Bwana ladumu milele."
Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. Maana,
"Wanadamu wote ni kama majani,
nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni;
majani hunyauka na maua huanguka,
lakini neno la Bwana ladumu milele."
Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
A inspiração divina
Toda Escritura é inspirada por Deus. Homens santos falaram da parte do Senhor, e a Palavra escrita é a expressão fiel da vontade divina.
Zaidi ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe. Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Mwana Ni Mkuu Kuliko Malaika
Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. Mwana ni mngʼao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni.
Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.
A Palavra como guia e tesouro
A Palavra de Deus é lâmpada para os pés, espada do Espírito e tesouro para o coração. Guardá-la e meditá-la nos protege do pecado.
Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
Utukufu Wa Mungu Katika Uumbaji
Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu,
anga zahubiri kazi ya mikono yake.
Siku baada ya siku zinatoa habari,
usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.
Hakuna msemo wala lugha,
ambapo sauti zao hazisikiki.
Sauti yao imeenea duniani pote,
nayo maneno yao yameenea
hadi miisho ya ulimwengu.
Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,
linafanana na bwana arusi
akitoka chumbani mwake,
kama shujaa afurahiavyo
kukamilisha kushindana kwake.
Huchomoza upande mmoja wa mbingu,
na kufanya mzunguko wake
hadi upande mwingine.
Hakuna kilichojificha joto lake.
Sheria ya Bwana ni kamilifu,
ikihuisha nafsi.
Shuhuda za Bwana ni za kuaminika,
zikimpa mjinga hekima.
Maagizo ya Bwana ni kamili,
nayo hufurahisha moyo.
Amri za Bwana huangaza,
zatia nuru machoni.
Maneno ya Bwana ni safi,
kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,
iliyosafishwa mara saba.
Ee Bwana, utatuweka salama
na kutulinda na kizazi hiki milele.
Lakini andiko lasemaje? "Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako," yaani, lile neno la imani tunalolihubiri.
Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana:
"Sauti yao imeenea duniani pote,
nayo maneno yao yameenea
hadi miisho ya ulimwengu."
Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.
Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.
na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.
Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli.