Publicidade

Proximidade

Por Bíblia Online

Deus é próximo dos que o buscam. Ele não é um Deus distante, mas presente, íntimo e acessível a todo o que o invoca com sinceridade de coração.

Buscar a presença de Deus

A Bíblia nos exorta a buscar a face do Senhor continuamente. Quem se aproxima dele encontra plenitude de alegria e delícias perpétuas.

Mtafuteni BWANA na nguvu zake,

Utafuteni uso wake sikuzote.

Mtafuteni BWANA na nguvu zake;

Utafuteni uso wake siku zote.

Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,

Mwiteni, maadamu yuko karibu;

Neno moja nimelitaka kwa BWANA,

Nalo ndilo nitakalolitafuta,

Nikae nyumbani mwa BWANA

Siku zote za maisha yangu,

Niutazame uzuri wa BWANA,

Na kutafakari hekaluni mwake.

Hakika siku moja katika nyua zako

Ni bora kuliko siku elfu kwingineko;

Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu,

Kuliko kuishi katika hema za uovu.

Utanijulisha njia ya uzima;

Mbele za uso wako kuna furaha tele;

Na katika mkono wako wa kulia

Mna mema ya milele.

Deus está perto

O Senhor está perto dos que o invocam, dos quebrantados de coração e dos que clamam por socorro. Sua presença nos sustenta.

Walilia, naye BWANA akasikia,

Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.

BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo,

Na huwaokoa waliopondeka roho.

Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yuko karibu.

Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.

Hakika wema na fadhili zitanifuata

Siku zote za maisha yangu;

Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

A presença que nunca abandona

Deus promete nunca nos deixar. Ele permanece fiel, está conosco em todo tempo e envia o Espírito para habitar em nossos corações.

Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

BWANA, Mungu wetu, na akae nasi, kama alivyokaa na baba zetu; asituache, wala asitutupe;

Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu mwenye neema na rehema.

Salamu za mwisho na baraka

Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

Salamu za mwisho na baraka

Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Naye alikuwa huko pamoja na BWANA siku arubaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.

waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.

Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi; naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi. Basi kwa siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati; lakini walipomgeukia BWANA, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao. Hata na zamani zile hakukuwa na amani kwake atokaye, wala kwake aingiaye, ila fadhaa kubwa juu yao wote wakaao katika nchi. Walivunjikavunjika, taifa juu ya taifa, na mji juu ya mji; kwa sababu Mungu aliwafadhaisha kwa shida zote. Nanyi jipeni nguvu, wala mikono yenu isilegee; kwa maana kazi yenu itakuwa na thawabu. Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaitengeneza upya madhabahu ya BWANA, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa BWANA. Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimjia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye. Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa. Wakamchinjia BWANA siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng’ombe mia saba, na kondoo elfu saba. Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta BWANA, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote; na ya kwamba yeyote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, awe ni mwanamume au mwanamke. Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa parapanda, na kwa baragumu. Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye BWANA akawastarehesha pande zote. Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea cheo chake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni. Lakini mahali pa juu hapakuondolewa katika Israeli; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu siku zake zote. Akavileta nyumbani mwa Mungu vitu alivyovitakasa babaye, na vile alivyovitakasa mwenyewe, fedha, na dhahabu, na vyombo. Wala hapakuwa na vita tena hata mwaka wa thelathini na tano wa kutawala kwake Asa.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-