Publicidade

Reino

Por Bíblia Online

O Reino de Deus é o tema central da pregação de Jesus. Desde o início de seu ministério, Ele proclamou: 'Arrependei-vos, porque é chegado o Reino dos céus.'

O anúncio do Reino

Jesus inaugurou seu ministério proclamando a chegada do Reino. Ele convida todos ao arrependimento e à fé nessa nova realidade.

Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: "Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia."

akisema, "Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema."

waponyeni wagonjwa waliomo na waambieni: Ufalme wa Mungu umekaribia.

Tazama jinsi miguu ya wale waletao habari njema

ilivyo mizuri juu ya milima,

wale wanaotangaza amani,

wanaoleta habari njema,

wanaotangaza wokovu,

wauambiao Sayuni,

"Mungu wako anatawala!"

A natureza do Reino

O Reino de Deus é governo soberano do Senhor sobre todas as coisas. Ele é o Rei eterno, imortal e invisível.

Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.

Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,

na utukufu na enzi na uzuri,

kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

ni chako wewe.

Ee Bwana, ufalme ni wako;

umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?

Ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;

yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Kwa kuwa Bwana ni mwamuzi wetu,

Bwana ndiye mtoa sheria wetu,

Bwana ni mfalme wetu,

yeye ndiye atakayetuokoa.

Bwana atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo Bwana mmoja na jina lake litakuwa jina pekee.

Entrar no Reino

Para entrar no Reino é preciso nascer de novo, tornar-se como criança e buscar primeiro a justiça de Deus acima de tudo.

Yesu akamjibu, "Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili."

Yesu akamwambia, "Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho.

Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.

Yesu akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa."

Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki,

maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni."

Cidadãos do Reino

Os cristãos são concidadãos dos santos e membros da família de Deus, chamados a viver dignamente do Reino que receberam.

Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni.

Utajiri Wa Mbinguni

"Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi Ufalme.

Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000.

Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-