Publicidade

Descansar no Senhor

Por Bíblia Online

Descansar no Senhor é um ato de fé. Em um mundo agitado, Deus nos convida a entregar nossas ansiedades, aquietar o coração e confiar plenamente em sua provisão e cuidado.

O convite ao descanso

Jesus convida os cansados e sobrecarregados a irem a Ele e encontrar descanso para as suas almas. O jugo dele é leve.

Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo

"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi."

Tulia mbele za Bwana

na umngojee kwa uvumilivu;

usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,

wanapotekeleza mipango yao miovu.

"Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu;

nitatukuzwa katikati ya mataifa,

nitatukuzwa katika dunia."

Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote,

miminieni mioyo yenu kwake,

kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

Confiança e paz

Quem confia no Senhor encontra paz perfeita. A ansiedade perde o poder quando entregamos tudo nas mãos do Deus soberano.

Utamlinda katika amani kamilifu

yeye ambaye moyo wake ni thabiti

kwa sababu anakutumaini wewe.

Hili ndilo Bwana Mwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:

"Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,

katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,

lakini hamkutaka.

Matunda ya haki yatakuwa amani,

matokeo ya haki yatakuwa utulivu

na matumaini milele.

bali wale wamtumainio Bwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.

Esperar no Senhor

Esperar no Senhor renova as forças. A Bíblia nos ensina que aquietar-se diante de Deus e confiar em seu tempo é marca da maturidade espiritual.

Mngojee Bwana,

uwe hodari na mwenye moyo mkuu,

nawe, umngojee Bwana.

Wimbo Wa Sifa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Nilimngoja Bwana kwa saburi,

naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

Mtwike Bwana fadhaa zako,

naye atakutegemeza,

hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

Katika hasira yako, usitende dhambi.

Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya

mkiichunguza mioyo yenu.

Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,

kwa yule ambaye humtafuta;

ni vyema kungojea kwa utulivu

kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

A fidelidade de Deus

Deus é fiel. Seus planos são de paz e esperança. Podemos descansar sabendo que Ele guarda e sustenta quem nele confia.

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Bwana, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

"Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika Bwana,

ambaye matumaini yake ni katika Bwana.

Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji

uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.

Hauogopi wakati wa joto ujapo;

majani yake ni mabichi daima.

Hauna hofu katika mwaka wa ukame

na hautaacha kuzaa matunda."

Bwana akajibu, "Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha."

Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

Mfalme akawaambia Yuda, "Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta Bwana Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupa raha kila upande." Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.

Hata walipokuwa wakiteremka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, "Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu." Naye mtumishi akafanya hivyo. "Lakini subiri hapa kwa kitambo kidogo, ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu."

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-